Saturday, December 29, 2012

Watu 8 wafariki nchini Kenya

 29 Disemba, 2012 - Saa 14:25 GMT

Familia zilizoathiriwa
Familia zilizoathiriwa kwa mujibu wa Gazeti la Standard Nchini Kenya wakipekuwa mali yao baada ya maporomoko hayo ya Ardhi
Watu wanane wamekufa baada ya nyumba kadha kufukiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la bonde la Kerio, magharibi mwa Kenya, jana usiku.
Maporomoko ya ardhi yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha katika bonde hilo. Eneo la Kerio pia limekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha.
Chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya kinasaidia jitihada za uokoaji na kutoa taarifa kwamba miili miili ya watu wanane imeonekana na watu wengine watano waliokolewa mapema leo.
Watu wengi hawana makaazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji au kufukiwa na maporomoko ya ardhi.

Friday, October 12, 2012

VURUGU ZA MAANDAMANO YA WAISLAMU MBAGALA KIZUIANI LEO

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakiandamana kupinga kitendo cha kijana Emmanuel Josephat anayedaiwa kukojolea Quran.
Barabara ikiwa imefungwa wakati wa vurugu hizo.
Wananchi wakishuhudia vurugu hizo.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia wakiwa na baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa katika vurugu hizo za maandamano.Wanausalama wakiwa kazini kuzuia vurugu hizo.

Saturday, October 6, 2012

ALICHO KIANDIKA DIAMOND KATIKA WEBSITE YAKE KUHUSIANA NA BRITHDAY YA WEMA SEPETU

Mwaka 1990, mwezi na siku kama ya leo Mrs. Abraham Sepetu ama (Mama Sepetu) alipata bahati ya kujifungua mtoto wa kike ambae alimtunuku jina la Wema Abraham Sepetu, Mtoto ambae Nyota yake ilianza kama masihara tu pale aliposhinda taji la Miss Tanzania 2006, kisha baadae kuingia katika Muvie Industry kama utaniutani vile na ghafla kuwa DIVA wa Tasnia hiyo, na licha tu ya udiva pia kuwa ICON wa Tanzania.Siku hii ya leo ya tarehe 28/09/ anazaliwa upya na kutimiza miaka 22.Honestly nina furaha sana na kila sababu yakusema "Happy Birthday Sepetu wa Sepetunga"....coz kiukweli ni mtu ambae kwa namna moja au nyinge anamchango mkubwa sana katika Mafanikio yangu hadi kufikia hapa nilipo, Sikuzote amekua akinipa Moyo, Motisha,Nguvu na kunisupport kwa hali na mali ili tu niweze kufika Mbali zaidi..toka kwenye "Upenzi" hadi leo kwenye "Cousins" mixer "Ushemlake" ni mbali sana nimetoka nae...narudia tena kusema nina BOOooonge la furaha na kila sababu ya kumwambia "Happy birthday Sepetu wa sepetunga" wish you all the best mama.....Maisha marefu yenye amani na Mafanikio tele..........wote tuseme Aaaamen!

Tuesday, October 2, 2012

THE LEGEND IS BACK


RICK ROSS: ASKARI MAGEREZA ALIYEGEUKA BILIONEA


WAKATI habari ya mjini ikiwa ni ujio wa mkali William Leonard Roberts II ‘Rick Ross’ kunako Tamasha la Serengeti Fiesta Bongo, Oktoba 6, 2012, usilolijua kuhusu mkali huyu ni kwamba aliwahi kuwa askari magereza (Correctional Officer) kwenye Gereza la Florida kwenye miaka ya 1990 kabla ya kugeukia gemu la Hip Hop alikotusua mkwanja wa maana.
Sababu za mkali huyo kutema mzigo wa magereza hazijawekwa wazi ingawa inadaiwa kuwa tatuu alizojichora, rekodi ya makosa ya jinai kama matumizi ya bunduki, kukutwa na kitu cha marijuana na mengineyo, vilisababisha asimamishwe mzigo, akaona isiwe tabu, mwaka 2002 akaingia kwenye Rap Game na kuanza kuchana mistari na kugeuka bilionea.

MAGARI MAWILI YAGONGANA NA KUWAKA MOTO MBALIZI MKOANI MBEYA, 10 WALIPOTIWA KUFARIKI DUNIA, MBUNGE WA VITI MAALUM MARY MWANJELWA ANUSURIKA, KATIBU WAKE ATEKETEA KWA MOTO


 HIVI NDIVYO MAAFA YALIVYO.

 GARI LILIVYO UNGUA MOTO BAADA YA AJALI.


 MAMIA YA WATU WALIOFIKA KUSHUHUDIA AJALI HIYO MBALIZI JIJINI MBEYA.


GARI HILI LILIVYOPINDUKA NA KUWAKA MOTO BAADA YA AJALI.
 MKUU WA MKOA WA MBEYA ALIYEVAA SUTI YA BLUU, MH. ABAS KANDORO AKIWA ENEO LA AJALI.
 HII NI GARI NYINGINE AMBAYO PIA ILIWAKA MOTO BAADA YA KUGONGANA.
 ZIMAMOTO WAKIWA ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUZIMA MOTO HUO.
 ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKIWA ENEO LA TUKIO AMBAPO AJALI HIYO IMESABABISHA VIFO VYA WATU KUMI.
 WATU WAKIWA WAMEONGEZEKA KUSHUHUDIA TUKIO HILI LA AJALI.
 MUONEKANO WA GARI HILI LIKIWA LIMEUNGUA LOTE.
MABAKI YA GARI HILI AMBALO NALO LILIUNGUA LOTE.
WANANCHI WAKIWA WANASHUHUDIA AJALI HUKU WENGINE WAKIWA WANAENDELEA KUOKOA MAJERUHI WA AJALI HIYO.
KIKOSI CHA FFU NAO WALIKUWEPO SAMBAMBA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UOKOAJI LINAENDA KIKAMILIFU.
PIA KATIKA ENEO HILI  MBUNGE WA VITI MAALUM MH.MARY MWANJELWA ALIKUWEPO NDANI YA PICK UP ILIYOUNGUA MOTO, KATIBU WAKE AMETEKETEA KWA MOTO NDANI YA GARI HILO.
HABARI KAMILI ITAWAJIA BAADAE.
 TONE MEDIA LIVE GROUP TUMESHUHUDIA TUKIO HILI.

TASWIRA ZA BASI LA DAR EXPRESS LIKITEKETEA KWA MOTO LEO ASUBUHI

Basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar likiteketea kwa moto eneo la Segera, mkoani Tanga leo asubuhi. Abiria wote 65 wamenusurika.

SUGU ADATA BAADA YA KUPATA MTOTO

UMESHAWAHI kuona mtu mzima amedata? Basi kwa taarifa yako habari za kupata mtoto, zilipomfikia Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, alitulia kama maji mtungini kwa muda, baada ya muda mfupi akaamka na kushangilia kwa nguvu, Showbiz inakumegea.
Kwa watu waliomzoea Sugu, walishangazwa na furaha yake, kwani ‘mudi’ yake ilikuwa juu mno baada ya kusoma SMS ya kumueleza kwamba yeye ni baba wa mtoto wa kike. Waliokuwa karibu yake, walipomuuliza, Sugu alitamka mfululizo: “My daughter, I’m now a father. My daughter, I’m the happiest MP right now.”
Alimaanisha: Binti yangu, sasa mimi ni baba. Binti yangu, sasa mimi ni mbunge mwenye furaha zaidi.
Jumatano iliyopita (Septemba 26, 2012) usiku, Sugu alipokea SMS kutoka kwa mzazi mwenzake, anayekwenda kwa jina la Faiza, asubuhi ya siku iliyofuata, hakuweza kuendelea kukaa Mbeya, alisafiri kwa mkoko wake wa heshima, Toyota Land Cruiser Amazon hadi Dar kumuona binti yake.
Mtoto huyo, Sugu amempa jina la Sasha-Desderia Joseph Mbilinyi. Kama ulikuwa hujafunuliwa, jina la Desderia ni la mama mzazi wa mbunge huyo, anayeitwa Desderia Mbilinyi ‘Mama Mbilinyi’.
Akizungumza na Showbiz, Sugu alisema: “Kwanza namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumpata Sasha-Desderia. Ni mtoto ambaye amekuja ndani ya mahitaji yangu. Yaani nilimhitaji na kweli amekuja.
“Kwa mama wa mtoto (Faiza), namuomba sana Mungu atujaalie maisha marefu yenye furaha na maelewano, tuweze kumlea mtoto wetu.”
Sasha-Desderia, ni mtoto wa kwanza wa Sugu ambaye mbali na ubunge, jina lake lipo juu kwa takriban miongo miwili sasa kutokana na harakati zake kwenye muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva, akiwa ameshatoa albamu 10, pamoja nyimbo zinazobamba zaidi ya 40.

WALIOVUNJA UCHUMBA WA WOLPER HAWA HAPA


Na Mwandishi Wetu
SIYO habari mpya kwamba ule uchumba wa kitajiri kati ya staa wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper Massawe na mfanyabiashara ‘mjanjamjanja’, Abdallah Mtoro ‘Dallas’ umevunjika, kinachotengeneza kichwa cha habari leo ni sababu iliyo nyuma ya kuachana kwao.
Uwazi ‘Mama wa Magazeti Pendwa’, linakuwa la kwanza kuanika sababu ya kuachana kwao, ikiwa ni kutaja majina ya watu ambao wamekuwa sababu ya kumwagana kwao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, sababu ya kwanza ni Wolper kuwa na hisia mbaya dhidi ya wanawake kadhaa, akiamini kwamba kuna kitu cha zaidi kati yao na Dallas.
Chanzo chetu kikataja majina ya watuhumiwa: “Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’, Halima Haroun ‘Halima Kimwana Manywele’, Khadija Shaibu ‘Dida’, Mohamed Ndama ‘Mtoto wa Ng’ombe’ na mwanamke mwengine aliyetajwa kwa jina moja la Sabaha.”
Kikafafanua sababu ya kila mmoja kutajwa: “Dida anatajwa kwa sababu moja kuu, kwa muda mrefu amekuwa akitambulika kama dada wa Dallas, kwa hiyo akawa anamwita Wolper wifi. Baadaye Wolper akawa na hisia mbaya na Dida, akaanza maswali.
“Kwa kawaida Dallas ni mtu asiyejali, kwa hiyo akawa anampotezea, yaani hampi majibu yaliyonyooka. Wolper alikuwa anataka kujua Dida ni dada yake Dallas kivipi? Kimjinimjini au ni ndugu kabisa. Wolper alipoona hakuna jibu la kunyooka, akaweka kinyongo, akawa hana imani na Dida.
“Wolper anaamini kwamba Dallas ametembea na Aunty Lulu, Halima Kimwana na Sabaha. Upande wa Ndama, Wolper alishamshtaki Ndama kwa kumtapeli. Sasa hivi Dallas na Ndama wapo pamoja, kwa hiyo Wolper anahisi anasalitiwa na mchumba wake. Mwisho akaona bora waachane.”
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa chanzo chetu, mwandishi wetu alizungumza na Wolper ambaye alikiri kuachana na Dallas, alipobanwa kuhusu sababu alikata simu, baadaye akaandika SMS: “Dallas ni mchafu, nimeshamfumania sana. Anatembea na wanawake hovyo.”
Alipopigiwa simu mara ya pili na kutakiwa kutaja majina ya wanawake ambao ameona wamekuwa na uhusiano na Dallas, hakuyaweka wazi ila alisema: “Nikiwazungumzia nitaonekana namuonea wivu, ila kwa kifupi Dallas amenidhalilisha. Ametembea mpaka na wanawake ambao siyo daraja langu kabisa.
“Mimi nilimheshimu Dallas, unajua alipokuwa nje alikuwa ananiheshimu kama mke wake mtarajiwa. Unajua mtu tabia yake utaijua mkiwa pamoja. Sasa aliporudi hapa na vitendo alivyofanya ndiyo nimeamini siyo mtu mzuri, hastahili kuwa mume wangu kabisa.
“Wakati mwingine nimekaa nyumbani, naambiwa Dallas yupo na wanawake. Navaa kininja, nakodi teksi, nikifika nashuhudia kila kitu halafu narudi nyumbani. Nimejionea mengi na mpaka sasa simhitaji tena. Nimeona wanawake zake, siyo hadhi yangu lakini kanichanganya nao.”
Aunty Lulu alipoulizwa alisema, hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dallas, akaongeza: “Tatizo Dallas anapenda sana utani, unaweza kukaa naye, watu wakija ananitambulisha mimi ni mke wake. Hilo ndiyo tatizo.”
Dida yeye alisema anashangaa kutajwa kwenye sakata la Wolper na Dallas kwa sababu ana zaidi ya miaka saba, hajakutana na mfanyabiashara huyo mjanjamjanja.
Halima Kimwana, Ndama na Dallas hawakupatikana lakini nafasi yao bado ipo ili nao waelezee kilichopo upande wao. Waandishi wetu bado wapo kazini wanawatafuta.

Thursday, September 27, 2012

FUMANIZI LAZUA JIPYAA..soma



Stori: Makongoro Oging'na Issa Mnally
LILE fumanizi la aina yake lililotokea wiki iliyopita kwenye gesti moja iliyopo Tabata - Segerea, Ilala jijini Dar limezua jipya!
Fumanizi hilo lilibuliwa na gazeti hili, Septemba 18, mwaka huu ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo walinaswa chumbani wakiivunja amri ya sita ya muumba.
MAPYAA NI HAYA
Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania akiwa na mumewe.
“Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.
Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
Habari za kufumaniwa kwa Judith zilitolewa katika gazeti hili toleo namba 727 la Septemba 20-26, 2012 likiwa na kichwa kisemacho; HILI NDO FUMANIZI.

CHUZ ADAIWA KUMSUSA MSANII WAKE MGONJWA

Stori: Na Gladness Mallya
MSANII mkongwe Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amemrushia lawama Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kwamba amemsusa baada ya kushikwa na ugonjwa wa kupooza.
Akizungumza kwa kuchanganya maneno kutokana na tatizo hilo, Mzee Kankaa alisema usiku wa Aprili 7, mwaka huu ndipo alipokumbwa na ugonjwa huo ambapo alipooza upande mmoja na kupoteza kumbukumbu.
“Baada ya kupatwa ugonjwa huu, Chuz ambaye nilifanya naye kazi kwa usahihi kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu ambayo kwa sasa ipo madukani, alifika kunijulia hali mara moja tu, tena kwa sekunde chache kisha akaondoka na hajawahi kurudi tena,” alisema kwa masikitiko mzee huyo.
Chuz alipopatikana kwa njia ya simu yake ya kiganjani, alikuwa na haya ya kusema: “Sijamsusa Mzee Kankaa, namheshimu sana tatizo mambo yalikuwa mengi ndiyo maana nikashindwa kwenda kumuona tena, lakini nitakwenda.”

Sunday, September 23, 2012

SHILOLE: KWA NILICHOKIONA, NIMEKOMA KUJICHUBUA

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Na Imelda Mtema
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.
Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.
“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:
“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.”

BABY MADAHA AMUIGA RIHANNA

Na Erick Evarist
MSANII anayefanya poa kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amefunguka kuwa anazimika na swaga za mwanamuziki kutoka Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’ hadi kufikia hatua ya kumuiga swaga zake.
Akizungumza na Mbovu Mbovu za Mastaa, amejikuta akifanya kila kitu anachokifanya mwanamuziki huyo kutokana na mapenzi aliyonayo kuanzia mavazi, kuimba na hata kucheza.