Nasib Abdul Juma ‘Diamond’.
Na Shakoor Jongo
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac
Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma
‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma, Ijumaa lina data
kamili.
Chanzo makini kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo
kwa paparazi wetu kwa njia ya simu juzi, ambapo kilisema ukaribu wao
uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku
Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All
Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo
mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema
alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa
msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa
mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond
ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake.
Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”
No comments:
Post a Comment