Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania
amewafuta kazi mawaziri waandamizi katika baraza lake la mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, waziri wa fedha Mustapha Mkullo ni miongoni mwa
waliowekwa kando.
Mawaziri wapya waliochukua nafasi mpya kuwapisha
walioachwa ni kama ifuatavyo (walioachwa majina kwenye mabano), Waziri
wa Nishati na Madini - Profesa Sospeter Muhongo (William Ngeleja),
Waziri wa Fedha - Dr William Mgimwa ( Mustapha Mkullo), Waziri wa
Uchukuzi - Dr Harrison Mwakyembe (Omar Nundu), Waziri wa Maliasili na
Utalii - Khamis Kagasheki (Ezekiel Maige), Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii - Dr Hussein Mwinyi (Dr Haji Mponda) na Waziri wa Viwanda na
Biashara - Dr Abdallah Kigoda (Dr Cyril Chami).Ubadhirifu
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambaye alibainisha hitilafu kadhaa za ubadhirifu wa fedha za umma kwenye wizara hizo.
Fedha za umma
Sura nyingi mpya zipo katika nafasi za manaibu waziri. Miongoni mwao ni January Makamba anayechukua unaibu waziri kwenye Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia, akina mama wawili Saada Mkuya Salum akiwa naibu waziri wa fedha kutokea Zanzibar bega kwa bega na mwenzake mpya Janet Mbene anayesimamia wadhifa huo huo kwa upande wa Tanzania bara.Vile vile Rais Kikwete kwa mara ya kwanza amewateua manaibu waziri wawili kusaidiana majukumu kwenye Wizara ya Nishati na Madini.
Mabadiliko hayo yamekuwa yakisubiriwa kwa muda tangu mjadala mkali ulipozuka bungeni kuwahusu mawaziri ambao wizara zao zilituhumiwa kuhusika na ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha fedha za umma.
Hata hivyo Rais Kikwete amewaeleza watanzania kuwa kuanzia sasa, uwajibika wa aina hiyo utawahusu maaafisa waandamizi wote katika wizara husika.
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI
OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Wataapishwa Jumatatu tarehe 8 Mei, 2012 saa 5.00 asubuhi katika viwanja vya Ikulu
No comments:
Post a Comment