Stori: Na Gladness Mallya
MSANII
mkongwe Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amemrushia lawama
Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kwamba
amemsusa baada ya kushikwa na ugonjwa wa kupooza.
Akizungumza kwa
kuchanganya maneno kutokana na tatizo hilo, Mzee Kankaa alisema usiku wa
Aprili 7, mwaka huu ndipo alipokumbwa na ugonjwa huo ambapo alipooza
upande mmoja na kupoteza kumbukumbu.
“Baada ya kupatwa ugonjwa huu,
Chuz ambaye nilifanya naye kazi kwa usahihi kwenye Tamthiliya ya Jumba
la Dhahabu ambayo kwa sasa ipo madukani, alifika kunijulia hali mara
moja tu, tena kwa sekunde chache kisha akaondoka na hajawahi kurudi
tena,” alisema kwa masikitiko mzee huyo.
Chuz alipopatikana kwa njia
ya simu yake ya kiganjani, alikuwa na haya ya kusema: “Sijamsusa Mzee
Kankaa, namheshimu sana tatizo mambo yalikuwa mengi ndiyo maana
nikashindwa kwenda kumuona tena, lakini nitakwenda.”
No comments:
Post a Comment