Monday, June 11, 2012

JOKATE NA DIAMOND MAPENZ UPYAA





Na Shakoor Jongo
SIKU kadhaa baada ya wapenzi mastaa, Miss Jokate Mwegelo na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’ kutibuana kisa kikiwa ni mwanamuziki huyo kunaswa hotelini na mwigizaji Aunt Ezekiel, wawili hao wamerudiana na kuanza mapenzi upya, Ijumaa Wikienda limeshiba data.
MAZUNGUMZO HOTELINI
Habari za uhakika kutoka kwa chanzo ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao zilieleza kuwa, baada ya kutokea kwa kutoelewana kati yao walikutana kwenye Hoteli ya Regency, Dar es Salaam ambapo walifanya mazungumzo kwa takribani saa 3.
MAZUNGUMZO YAZAA MATUNDA
Chanzo hicho kilidai kuwa mazungumzo hayo ndiyo yaliyozaa matunda kwani walikubaliana kuanza mapenzi upya na wakaweka mikakati kujiimarisha kisanaa.
“Kama hamniamini muulizeni…(anatajwa mwigizaji ambaye pia ni mtangazaji), alikuwa ameweka kambi pale Regency Hotel kwa ajili ya filamu yake mpya. Alishuhudia mpango mzima,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Nusura Almasi (Diamond) atoe chozi, ndipo Jokate akamsamehe na sasa anapiga pamba za Kidoti tu (zinabuniwa na Jokate).”
JOKATE, HASHEEM
Kwa mujibu wa chanzo kingine, Jokate alikubali kurejea kwa Diamond baada ya ile skendo ya kudaiwa kufungiwa vyoo vya gari aina ya Hummer na staa wa kikapu wa NBA, Hasheem Thabeet walipokutana hivi karibuni pale Diamond Jubilee, Dar, jamaa akiwa na ‘kifaa’ kingine.
DIAMOND FUNGUKA
Ili kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda lilimsaka Diamond kwa niaba ya ‘kapo’ yao ili afunguke ambapo alikiri kukaa chini na Jokate na kumaliza tofauti zao.

No comments:

Post a Comment