Thursday, September 27, 2012

FUMANIZI LAZUA JIPYAA..soma



Stori: Makongoro Oging'na Issa Mnally
LILE fumanizi la aina yake lililotokea wiki iliyopita kwenye gesti moja iliyopo Tabata - Segerea, Ilala jijini Dar limezua jipya!
Fumanizi hilo lilibuliwa na gazeti hili, Septemba 18, mwaka huu ambapo Judith Lekule na mume wa mwanamke aliyetambuliwa kwa jina moja la Pendo walinaswa chumbani wakiivunja amri ya sita ya muumba.
MAPYAA NI HAYA
Kwa mujibu wa vyanzo, Judith yu mbioni kwenda kortini kwa lengo la kumfungulia mashitaka Pendo akidai alimdhalilisha kwa kudai alimfumania akiwa na mumewe.
“Kuna watu wanamshawishi Judith eti asikae kimya, aende mahakamani akamshitaki Pendo kwamba alimdhalilisha kusema alimfumania na mumewe,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, vyanzo vimeeleza kwamba, Judith anashindwa kuutumia ushauri huo kutokana na ukweli kwamba, kesi hiyo inaweza kumgeukia mwenyewe kwa sababu yeye ndiye aliyefumaniwa.
Sambamba na madai hayo, inasemekana pia kwamba mtaani anapoishi Judith kumekuwa kuchungu kwake baada ya baadhi ya watu kutumia habari ya kwenye gazeti kumkejeli na kumuonya akome kuwadandia waume za watu kwani si tabia nzuri.
“Hali hiyo ya kunyooshewa vidole na watu inamnyima raha Judith, anashindwa kutembea kwa uhuru mitaani,” alisema mnyetishaji wetu.
Nao baadhi ya marafiki wa kike wa Judhith wamehuzunishwa na kitendo cha mwenzao kufumaniwa na kupewa kipigo.
Chanzo kikaenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, ndugu wamemtaka Judith aondoke anapoishi kufuatia kitendo alichokifanya ikielezwa ameitia aibu familia.
Kwa upande wake, Pendo ameeleza kwamba mumewe alimuomba msamaha na amemsamehe, yameisha pia akasema baada ya lile fumanizi, Judith amemfuata nyumbani kwake mara mbili kwa lengo la kuomba msamaha.
“Nimemsamehe Judith lakini bado ana wasiwasi kwani amekuwa akija kwangu na hofu kwamba nitamshitaki katika vyombo vya sheria.
“Cha ajabu sasa amegeuka na kutoa vitisho, Judith ni rafiki yangu, anajua alichokifanya ndiyo maana hata wapambe wake wanamshawishi akanishitaki lakini moyo wake unakuwa mgumu,” alisema Pendo.
Habari za kufumaniwa kwa Judith zilitolewa katika gazeti hili toleo namba 727 la Septemba 20-26, 2012 likiwa na kichwa kisemacho; HILI NDO FUMANIZI.

CHUZ ADAIWA KUMSUSA MSANII WAKE MGONJWA

Stori: Na Gladness Mallya
MSANII mkongwe Bongo, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amemrushia lawama Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kwamba amemsusa baada ya kushikwa na ugonjwa wa kupooza.
Akizungumza kwa kuchanganya maneno kutokana na tatizo hilo, Mzee Kankaa alisema usiku wa Aprili 7, mwaka huu ndipo alipokumbwa na ugonjwa huo ambapo alipooza upande mmoja na kupoteza kumbukumbu.
“Baada ya kupatwa ugonjwa huu, Chuz ambaye nilifanya naye kazi kwa usahihi kwenye Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu ambayo kwa sasa ipo madukani, alifika kunijulia hali mara moja tu, tena kwa sekunde chache kisha akaondoka na hajawahi kurudi tena,” alisema kwa masikitiko mzee huyo.
Chuz alipopatikana kwa njia ya simu yake ya kiganjani, alikuwa na haya ya kusema: “Sijamsusa Mzee Kankaa, namheshimu sana tatizo mambo yalikuwa mengi ndiyo maana nikashindwa kwenda kumuona tena, lakini nitakwenda.”

Sunday, September 23, 2012

SHILOLE: KWA NILICHOKIONA, NIMEKOMA KUJICHUBUA

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Na Imelda Mtema
MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.
Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea matatizo kwenye mwili wake.
“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:
“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.”

BABY MADAHA AMUIGA RIHANNA

Na Erick Evarist
MSANII anayefanya poa kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amefunguka kuwa anazimika na swaga za mwanamuziki kutoka Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’ hadi kufikia hatua ya kumuiga swaga zake.
Akizungumza na Mbovu Mbovu za Mastaa, amejikuta akifanya kila kitu anachokifanya mwanamuziki huyo kutokana na mapenzi aliyonayo kuanzia mavazi, kuimba na hata kucheza.

BASATA WAMJIA JUU AUNT EZEKIEL..PICHA ZA AIBU HIZI HAPA


Stori: George Kayala
SAGA la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel (pichani) kuvaa nusu utupu na kukaa kihasara huku maungo nyeti yakichungulia, limechukua sura mpya baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumjia juu, Ijumaa Wikienda linafunguka.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego, wasanii wamekuwa wakionywa mara kwa mara kuhusu kuzingatia maadili na kuacha kuvaa nguo za nusu uchi hivyo inapotokea mmoja wao akawa kichwa ngumu, basi huyo atakuwa na ugonjwa akilini hivyo anahitaji ushauri wa kisaikolojia.
“Huyo Aunt Ezekiel anahitaji ushauri nasaha kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa watu wengine wenye tatizo kama lake. Anapaswa kusikiliza maelekezo ya Basata kwamba nguo zisizo na maadili ya Mtanzania hazitakiwi katika sanaa yetu, aache mara moja.
“Kila Jumatatu huwa tuna Jukwaa la Sanaa hivyo tumeshakutana na wasanii hao na kuwaeleza tatizo hilo lakini wamekuwa wagumu wa kuelewa. Tumeona njia pekee ya kuwasaidia ni kuwapa ushauri wa bure juu ya madhara ya kuvaa nguo hizo,” alisema mkurugenzi huyo kwa staili ya kumpa onyo kali msanii huyo.
Hivi karibuni, Aunt akiwa kwenye ziara ya Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mkoani Mwanza alijikuta akilewa na kushindwa kujisitiri kutokana na kigauni alichokuwa amevaa kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maumbile yake muhimu.

Afande aacha kazi ya ulinzi uwanjani na kugeuka paparazi‏mmCheki alichokifanya

Afande akipiga picha kwa kutumia simu yake
Hapa akimpiga picha aliyekuwa kocha wa yanga Tom Saintfiet kabla ya kutimuliawa
Askari mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya Yanga, Jumatano iliyopita alilazimika kuacha kazi ya ulinzi na kusukumana na mapaparazi akiwapiga picha wachezaji na kocha wa Yanga kwa kutumia kamera ya simu yake.
Baadhi ya maaskari wa Tanzania ni mashabiki wakubwa wa timu za Simba na Yanga na kujikuta wakionyesha mapenzi yao bila kujali kama wako kazini, katika mchezo huo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Yanga uliopigwa Jumatano iliyopita ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogororo, Yanga ilichapwa bao 3-0, ambapo miongoni wa watu walioonekna kusononeka na kichapo hicho ni Afande huyo wa kikosi cha kutuliza ghasia.
Mashabiki wa Simba waliopata kumshuhudia kijana huyo wa I.G.P Said Mwema walimzomea na kumtupia maneno ya kejeli hali iliyomfanya kusitisha zoezi hilo na kuweka simu yake mfukoni na kuchukua kilungua chake na kuendelea na kazi.                 
PICHA HABARI NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL MOROGORO

Saturday, September 22, 2012

KUFURU YA UTAJIRI BONGO

Hoteli ya Singita Grumeti Reserves.
Stori: Mwandishi Wetu
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.
Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
Hoteli hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Matokeo hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi, matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari, vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani (Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais, matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni na kadhalika.

HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake zinazotikisa duniani.
Bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye hoteli hiyo.
Bilionea wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani, alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya 19.
Mke wa zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole, Cheryl, alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba alifikia kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno, tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za kiusalama.

SIFA ZA HOTELI HIYO
Ni hoteli yenye eneo kubwa, kutoka ‘loji’ moja hadi nyingine, inabidi utumie usafiri maalum.
Imegawanywa kwenye ‘loji’ mbili, moja inaitwa Ebony na nyingine ni Boulder.
Hoteli hiyo, pia inaundwa na ‘loji’ nyingine inayoitwa Castleton Camp ambayo inaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Bei ya chini kabisa kwa mtu kulala kwenye hoteli hiyo ni shilingi 2,000,000 na bei hiyo hutegemea na msimu.
Bei zimetofautiana kati ya ‘loji’ moja hadi nyingine na mtu kulala kwenye Castleton Camp, inaweza kugharimu mpaka shilingi milioni 23 kwa siku moja.
Singita Grumeti ni moja kati ya hoteli za Singita za nchini Afrika Kusini.