Askari mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya
Yanga, Jumatano iliyopita alilazimika kuacha kazi ya ulinzi na
kusukumana na mapaparazi akiwapiga picha wachezaji na kocha wa Yanga kwa
kutumia kamera ya simu yake.
Baadhi ya maaskari wa Tanzania ni
mashabiki wakubwa wa timu za Simba na Yanga na kujikuta wakionyesha
mapenzi yao bila kujali kama wako kazini, katika mchezo huo wa mzunguko
wa pili wa ligi kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Yanga
uliopigwa Jumatano iliyopita ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mkoani
Morogororo, Yanga ilichapwa bao 3-0, ambapo miongoni wa watu walioonekna
kusononeka na kichapo hicho ni Afande huyo wa kikosi cha kutuliza
ghasia.
Mashabiki wa Simba waliopata kumshuhudia
kijana huyo wa I.G.P Said Mwema walimzomea na kumtupia maneno ya kejeli
hali iliyomfanya kusitisha zoezi hilo na kuweka simu yake mfukoni na
kuchukua kilungua chake na kuendelea na kazi.
PICHA HABARI NA DUNSTAN SHEKIDELE, GPL MOROGORO
No comments:
Post a Comment