Monday, July 23, 2012

UTAPELI WA CHUZ, DAVINA ATAJWA


Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’.

Halima Yahya ‘Davina’.
Stori: Mwandishi Wetu
LILE sakata la bosi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ kudaiwa kuingia mitini na ‘mafweza’ ya ndugu wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Itien Kabila kiasi cha Sh. milioni 500 limefungukia ukurasa mwingine ambapo mwigizaji ‘seksi’ Bongo, Halima Yahya ‘Davina’ anadaiwa kufahamu mchongo mzima.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Davina ndiye mtu wa kati katika sakata hilo ambapo yeye alikuwa shahidi wa Chuz kukopeshwa kiasi hicho cha fedha na alikula kitu kidogo kama ‘macho kuona’.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Davina na kumuuliza kama taarifa hizo zina ukweli wowote ambapo aliruka kimanga akisema: “Akha! Mi simjui huyo Kabila, nani kawaambia?”
Chuz alipopigiwa simu juzi Jumamosi na kuulizwa kuhusu ushiriki wa Davina, alikiri kufahamu yeye kukopeshwa fedha hizo lakini akasema msanii huyo si shahidi wala hakulipwa fedha yoyote.
Aliongeza: “Lakini mbona mmekomalia ishu ambayo hainihusu, kuna nini kwani jamani? Yeye si kasema ataizuia filamu yangu ya Dirty Game, afanye hivyo kama ana ubavu.”

MAAJABU AJALI ZA MELI...SOMA



Stori: Mwandishi Wetu
MELI ya MV Skagit imekwishazama kabisa kwenye Bahari ya Hindi eneo ambalo ilitokea ajali na zoezi la kutafuta maiti nyingine limesitishwa, serikali ilisema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tamko hilo la serikali lilikuja huku ndugu wa watu ambao hawakupatikana wakiwa wanaumia kwa majonzi yasiyo na kifani kufuatia akili zao kushindwa kuamini kama kweli ndugu zao hawataonekana walikolala.
Baadhi ya watu waliozungumza na Ijumaa Wikienda, pia wameshangazwa na maajabu yanayotokana na kuzama kwa meli, vifo vya abiria na zoezi la uokoaji.
Wengi wanaamini kwamba ajali za meli huambatana na maajabu kwani haijawahi kutokea maiti wote kupatikana hata kama kukiwepo na wapiga mbizi maarufu wa dunia.
“Ajali ya MV Taitanic iliyozama miaka ya tisini, MV Bukoba mwaka 96, MV Spice Islanders, mwaka jana, MV Skagit na nyingine nyingi, abiria hawakupatikana wote. Ni lazima wengine wabaki,” alisema Maulid, mkazi wa Kariakoo, jijini Dar ambaye mke wa rafiki yake hakuonekana katika ajali hiyo.
Kikubwa walichosema wananchi baada ya serikali kutoa tamko hilo ni kwamba, inauma sana. Afadhali nduguyo afe umuone, umuhifadhi kaburini hata kama amekatika mikono yote kuliko kutomuona tena maisha.
Mpaka Jumamosi iliyopita, waliookolewa kwenye ajalio hiyo ni watu 146, maiti zilizoopolewa ni 68 huku watu wanaokadiriwa kufikia zaidi ya mia moja wakibaki ndani ya meli hiyo.

MAGAZETI YA LEO; WABUNGE WAPONDWA, WABUNGE WAMSAFISHIA ZITTO NJIA YA URAIS 2012 NA MGAO MKALI UMEME WAJA

Monday, July 23, 2012


Friday, July 20, 2012

KUTOKA KWENYE BLOG HADI WEBSITE "SINTAH"

Mwanadada machachari wa bongo movie anajulikana kwa jina la Sintah aka JLO wa bongo baada ya kufungua blog yake na kuwa gumzo la jiji sasa ameamua kupiga step kidogo na kuhamia kwenye website. Mwenyewe anasema ukitaka kupata burudani na kumjua zaidi basi usisite kumtembelea katika website yake ambayo ni hii hapa www.sintah.com

HEMED NA MLELA USO KWA USO NDANI YA RED CROSS!


Shilole chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani


Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Na Imelda Mtema, Zanzibar
MSANII wa filamu na muziki wa Pwani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameponea chupuchupu kuvuliwa nguo barabarani maeneo ya Darajani mjini hapa baada ya kukatiza mitaa ya sokoni akiwa katupia kigauni kifupi ajabu.
Bongowood ilimshuhudia Shilole akiwa na wanenguaji wake akipigiwa kelele na wanaume waliotaka kumkamata wamvue kisha wamlambe viboko hivyo akalazimika kukimbilia dukani akanunua dela na kulivaa juu ya kigauni cha kihasara alichokuwa amekitinga.

TATUU ZA QUEEN SUZY WA NGWASUMA ZAPAGAWISHA MASHABIKI MORO

Baadhi ya tatuu za Queen Suzy.
...Akionyesha machejo jukwaani.
Mwandishi wa mtandao huu akimhoji Suzy (katikati).  Kulia ni mnenguaji mwenzake.
...Akionyesha matindo ya aina yake kwa kupiga msamba.
...Akijtayarisha  kuonyesha tatuu zake za nyuma.
MNENGUAJI nyota wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma',  Suzan Godwin Chubwa  'Queen Suzy' hivi karibuni alipagawisha mashabiki katika Manispaa ya Morogoro wakati wa hafla ya kumtafuta Miss Morogoro kutokana na tatuu zake maridadi alizojichora mwilini.
Hafla hiyo ilifanyika Morogoro Hotel.
Akizungumza na mtandao huu, mrembo huyo ambaye kabla ya kujiunga na bendi hiyo alikuwa na bendi ya African Stars wajulikanao kama ‘Twanga Pepeta’, alisema mapambo hayo ni kwa ajili ya kuwachengua mashabiki  wake wakati akinengua jukwaani.

RAIS KIKWETE ATUA ZANZIBAR KUFARIJI WALIOPATWA NA AJALI YA MELI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana Julai 19, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali jana Julai 19, 2012.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja jana Julai 19, 2012.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi jana Julai 19, 2012.

(PICHA NA IKULU)

DOTNATA ABADILI DINI





Husna Posh ‘Dotnata’.
Hamida Hassan na Gladness Mallya
MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu za Kibongo, Husna Posh ‘Dotnata’ amebadili dini kutoka Uislam na kuwa Mkristo kwa kile alichodai ni kutengeneza maisha yake baada ya kuhangaika na mambo ya dunia kwa muda mrefu.
Akichezesha taya na Ijumaa, Dotnata alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuugua na kuhangaika kwa waganga wengi kwa muda mrefu bila ya mafanikio.
Dotnata ametaja sababu nyingine ni mama yake mzazi ambaye alifikia hatua ya kususa kumtembelea nyumbani kwake hasa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani akimtaka aokoke.
“Mama alinipa masharti kwamba nitakapookoka ndipo atakapofika kwangu jambo ambalo lilikuwa linaninyima amani na kunifanya nichukue uamuzi huo,” alisema.
Dotnata ambaye awali alikuwa ni Mkristo amebatizwa upya na anatumia jina lake la awali kabla ya kuwa Muislam la Iluminata na amejiunga na Kanisa la Ufufuo na Uzima (kwa Gwajima) lililopo Kawe jijini Dar.
“Nitakuwa nahudhuria kanisani siku tatu kwa wiki kwa ajili ya kujifunza neno, pia nyumbani kwangu nimetenga sehemu maalum kwa ajili ya kuangalia mahubiri ya mtumishi wa Nigeria TB Joshua kwa njia ya runinga,” alisema.
Dotnata amesema kuwa ameapa kutogeuka tena kwani ataendelea na wokovu wake mpaka dakika ya mwisho wa maisha yake ili atakapozikwa ndugu na jamaa zake wacheze sebene la Yesu.
“Naomba niliowakosea wanisamehe kwani wengine nimeshawapigia simu na kuwaomba radhi, hivyo natumia fursa hii kuwaomba wengine wote wanisamehe kwa sababu nimeanza maisha mapya,” alisema Dotnata.
Alipoulizwa kuwa mumewe Posh amelipokea vipi suala la kuokoka kwake, Dotnata alisema mumewe hana matatizo na anaona ni jambo la kawaida na maisha ya upendo na amani yanaendelea kutawala ndani ya ndoa yao.

WEMA, DIAMOND WANASWA KIGOMA

Nasib Abdul Juma ‘Diamond’.
Wema Isaac Sepetu.
Na Shakoor Jongo
STAA wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu na kichwa kinachotingisha katika Bongo Fleva, Nasib Abdul Juma ‘Diamond’ wamenaswa wakiwa beneti mkoani Kigoma, Ijumaa lina data kamili.
Chanzo makini kilichopo mkoani humo, kimepenyeza habari hiyo kwa paparazi wetu kwa njia ya simu juzi, ambapo kilisema ukaribu wao uliamsha hisia kwamba huenda wawili hao wamerudiana.
“Wapo wote huku Kigoma, kwa Diamond ni sawa maana yupo na wasanii wenzake wa Kigoma All Stars, sasa Wema amekujaje? Kwanza siyo mwanamuziki, lakini pia siyo mtu wa Kigoma ni wa kutoka Tabora,” kilieleza chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hiyo, Ijumaa lilimvutia waya Diamond zaidi ya mara tatu lakini simu iliita bila kupokelewa.
Wema alipopigiwa simu alipatikana na kufafanua ishu nzima ilivyo. Huyu hapa msikie: “Ni kweli nipo huku Kigoma lakini sipo na Diamond. Nimekuja kwa mwaliko wa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini).
“Mimi na Diamond ni marafiki tu, hatuwezi kuwa wapenzi tena, kila mtu na maisha yake. Kifupi nina mtu wangu ambaye tunapendana na kuheshimiana sana.”
Alipotakiwa kumtaja mpenzi wake mpya alisema: “Kwa sasa siwezi kumtaja, lakini siku si nyingi nitamuweka hadharani watu wamjue.”

Tuesday, July 10, 2012

DIVA LOVENESS LOVE ATAKAENIOA MAHARI SI CHINI YA MILIONI 500

Tuesday, July 10, 2012

Mwana dadiva anaeendisha kipindi cha ala za roho ndani ya the people's station Diva loveness love jana amefunguka alipokuwa akifanya kipindi cha xxl na mtu mzima Adam Mchomvu kuwa kwa yeyote atakae jitokeza kumuoa basi lazima awe na si chini ya shilingi millioni 500

MAPAJA YA UWOYA YAMLIZA MCHIMBA MADINI



 Irene Uwoya.
 Mchimba madini .
Stori: Imelda Mtema, aliyekuwa Mererani
MAPAJA ya mcheza filamu mkali Bongo, Irene Uwoya yamemtoa machozi mchimba madini maarufu ‘Mwanaapolo’ wa mgodi wa Florida uliopo Mererani, Manyara.
Tukio hilo ambalo ni sawa na kituko, lilijiri hivi karibuni wakati staa huyo na wenzake wa Bongo Movie walipotinga eneo hilo kwa ajili ya uzinduzi wa filamu moja ya msanii mwenzao.
Ilikuwa wakati wasanii hao wakiingia kwenye mgodi huo kwa lengo la kujifunza uendeshaji wake kuanzia kuchimba madini, ilipofika zamu ya Uwoya, sauti ya kilio kikubwa ilisikika kutoka kwa Mwanaapolo huyo aliyejulikana kwa jina la Hamad Hussein.
“Aaaash! Weweeee! Weeee, dada unaniumiza wewe, dadaaa jamani,” alisema mchimba madini huyo akimkazia macho Uwoya huku wenzake wakishangilia kumuunga mkono.
Njemba huyo aliendelea kupiga kelele huku akivua kofia na shati hali iliyomfanya paparazi wetu amfuate kumuuliza kulikoni.
“Hapana dada, niache tu yule dada ni mzuri. Sijawahi kuona mwanamke mwenye mapaja mazuri kama huyu, nipo hapa kwa zaidi ya miaka minne. Sasa jamani amenichanganya, navua nguo zote sasa hivi siwezi kuvumilia,” alisema Hamad huku akilia.
Baada ya Irene kutoka shimoni, jamaa huyo alipaza sauti tena na kumrushia kofia Irene ili aivae lakini kwa bahati mbaya staa huyo alishaingia ndani ya gari na kwenda kwenye mgodi mwingine.

KISANGA GARI LA WOLPER



Gari la Wolper aina ya BMW X6.
Jacqueline Masawe ‘Wolper’.
Na Gladness Mallya
SAKATA la kukamatwa kwa lile gari la kifahari aina ya BMW X6 lenye thamani ya takriban Sh. milioni 175 la staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe limeibua kisanga kipya, Ijumaa lina kila kitu mkononi.HABARI BILA WASIWASI
Habari bila wasiwasi zimeeleza kuwa pedeshee maarufu jijini Dar es Salaam, Mohamed Ndama a.k.a Ndama Mtoto wa Ng’ombe ndiye aliyemwingiza Wolper mkenge hivyo jamaa huyo ametiwa mbaroni akidaiwa kuhusika kuliingiza Bongo kinyemela.
Kwa mujibu wa chanzo kisichokoroma ambacho ni rafiki mkubwa wa Wolper, Ndama aliwekwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Kati (Central), Dar Jumanne wiki hii baada kutajwa kuwa alihusika na uingizaji wa gari hilo hapa nchini.
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa mchumba wa Wolper, Abdalla Mtoro ‘Dallas’ au Rais wa Ununio alitoa fedha kwa pedeshee huyo na kumtaka atafute gari la kifahari kwa ajili ya mchumba’ke (Wolper).
GARI LENYE HADHI YA WOLPER
Kilidai kuwa katika kutafuta gari lenye hadhi ya Wolper ndipo akampatia mwigizaji huyo lile BMW X6 na kubandikwa namba za usajili T 574 BXF.
TURUDI NYUMA KIDOGO
Katika habari ya kukamatwa kwa gari hilo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, ilielezwa kuwa lilikamatwa kwa sababu liliingizwa nchini bila vibali husika na pia kudaiwa ushuru unaokadiriwa kufikia Sh. milioni 70.
TUENDELEE NA CHANZO
“Unajua Ndama aliwapiga changa la macho Wolper na Dallas kwa sababu alipewa madaraka yote ya kutafuta gari hilo la kifahari.
“Ilikuwa ni vigumu kwa Wolper kutia shaka kwa sababu alipokabidhiwa lilikuwa na ‘dokumenti’ zote na ndiyo maana akawa anatanua nalo bila wasiwasi, lakini ndo hivyo ngoja tuone itakuwaje,” kilisema chanzo chetu cha kuaminika na kuongeza:
“Jumanne ndiyo aliitwa Central akahojiwa kwa saa kadhaa na Wolper akiwepo.
“Baada ya mahojiano pale kituoni hadi jioni ndipo akatupwa ‘lokapu’.
“Sijui kama alitoka kwa dhamana au alilala pale kituoni, fuatilieni.”
Baada ya kumwagiwa data, Ijumaa liliingia mzigoni ndipo likafanikiwa kupata ukweli kuwa Ndama alifunguliwa jalada la kesi namba CD/RB/7005/2012 na CD/IR/2624/2012.
KOVA ANASEMAJE?
Jumatano wiki hii, Ijumaa lilifunga safari hadi ofisini kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ili kulizungumzia tukio hilo lakini jitihada ziligonga mwamba baada ya kumsubiri muda mrefu kwa maelezo kwamba alikuwa kwenye kikao nyeti.
WOLPER ANAKATAKATA
Alipotafutwa Wolper alikuwa akikatakata simu kila alipopigiwa kwenye kilongalonga chake cha kiganjani.
TUMEFIKAJE HAPA?
Gari la Wolper lilikamatwa Juni 28, mwaka huu na kampuni ya Mnada ya Majembe kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuingizwa nchini kinyemela na kutolipiwa ushuru kwa muda wa miaka 5.

Monday, July 9, 2012

WEMA SEPETU, JACQUELINE WOLPER HAKUNA MBABE...picha na matukio

Mwamuzi akiamua mpambano uanze.
...Ngumi ndo zinaanza.
...Wolper akimkabili Wema.
...Wakishikana.
...Wakizidi kuonyeshana umwamba.
....Ndonga zikiendelea.
...Mpambano ukiwa umekolea.
...Wema akipata mawaidha kutoka kwa mwalimu wake Rashid Matumla.
....Picha ya pamoja baada ya mpambano huo uliomalizika kwa suruhu.
Waigizaji mahiri wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper walitoka suruhu katika mpambano wao wa raundi 2 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini Juni 7, 2012.

Friday, July 6, 2012

CHRIS BROWN AKIPARTY NA GIRLFRIEND WAKE KARRUECHE TRAN HOLLYWOOD

Friday, July 6, 2012


Ilikuwa ni furaha kwa Chriss baada ya kuachia album yake inayoitwa FORTUNE na pia kwa kupiga show kali kwenye BET awards



WOLPER: NAJIFUA NIMCHAKAZE WEMA..PICHA NA MATUKIO

Thursday, July 5, 2012




HII ni burudani nyingine ya aina yake ambayo itapatikana katika tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7, Uwanja wa Taifa jijini Dar. Nazungumzia mpambano wa masumbwi kati ya mashostisto wawili maarufu Bongo, Jacqueline Wolper na Wema Sepetu, ebwana eee! Haijawahi kutokea.
Kamera yetu hivi karibuni iliwanasa mwanadada Wolper na bondia Rashid Matumla wakila tizi kwa nguvu zote, pande za Mbezi Beach yalipo maskani ya Wolper, ikiwa ni maandalizi ya pambano hilo litakalokuwa na raundi sita. Wolper alipoulizwa kulikoni amevaa gloves na kusukuma punching bag kama hana akili nzuri, alifunguka kuwa anajiandaa kumchakaza Wema.
“Natafuta pumzi na stamina ya kutosha, si unajua mbele yangu kuna pambano kali dhidi ya adui yangu Wema. Nataka nimshikishe adabu ili tuheshimiane,” alisema Wolper

RAY aichomolea ndoa


Vincent Kigosi ‘Ray’.

STAA wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameweka wazi kuwa watu wanaomsumbua juu ya suala la kuoa, watasubiri sana kwani hana mpango huo.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Ray alifunguka kuwa staili ya maisha yake ndiyo inayomfanya aishi anavyotaka hivyo suala la kuoa halipo kwenye akili yake.
Alisema amekuwa akishauriwa na ndugu, jamaa na marafiki afanye hivyo ili yasije yakamkuta kama yaliyomkuta swahiba wake marehemu Steven Kanumba aliyefariki dunia akiwa hajaoa wala hana mtoto lakini yeye hana mzuka na mambo hayo.
“Sina mpango wa kuoa bwana, wanaotaka kuoa waoe tu na mimi nitachangia michango lakini mimi sipo tayari kwa sasa,” alisema Ray ambaye sasa ana umri wa miaka 32.

Monday, July 2, 2012

KANYE WEST, JAY – Z, BIG SEAN CHRISS BRIZZ WATISHA B.E.T 2012.

Monday, July 2, 2012


.
Usiku wa Jumapili iliyopita Big Sean aliperform kwenye tuzo za B.E.T na Kanye west 2 Chainz na Pusha T. Alipata tunzo ya Best New Artist, Jay – z na Kanye West wakachukua tunzo ya Video of the year “Ortis” Diggy Simmons alichukua tunzo ya Younstar Award, Chriss Brown alichukua tunzo ya “Best Male R&B Artist Msanii mburudishaji wa mwaka. Beyonce alishinda tuzo ya Video Director wa mwaka akiwa na Alan Ferguson na ngoma ya “Party” na Best Female R&B Artist wakati Wale na Miguel wakashinda tuzo ya “Lotus Flower Bomb”  na Nick Minaj alishinda kama Best Female Hip-Hop Artist.
Kama vipi check list nzima chini :-

Centric Award
Common
Younstars Award
Diggy
Best Group
The Throne (Jay-Z and Kanye West)
Best Actor
Kevin Hart, "Think Like a Man"
Best New Artist
Big Sean
Best Male R&B Artist
Chris Brown
Best Collaboration
Wale (featuring Miguel), "Lotus Flower Bomb"
Best Gospel
Yolanda Adams
Best Female R&B Artist
Beyoncé
Best Female Hip-Hop Artist
Nicki Minaj
Lifetime Achievement Award
Maze, featuring Frankie Beverly
Video of the Year
The Throne (Jay-Z and Kanye West), featuring Otis Redding, "Otis"
Humanitarian Award
The Reverend Al Sharpton
Viewers' Choice Award
Mindless Behavior
Video Director of the Year
Beyoncé and Alan Ferguson
Entertainer of the Year
Chris Brown
.

UWOYA AKIRI KUPOTEZA MWELEKEO

Irene Pancras Uwoya.
Na Imelda Mtema
MWIGIZAJI Irene Pancras Uwoya amekula kiapo mbele ya Ijumaa Wikienda kuwa hataki kuonja pombe tena kwani anakiri zimempotezea mwelekeo kwa kumharibia vitu vyake vingi.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati, Uwoya ambaye ni mke wa ndoa wa mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’, alisema amegundua kuwa pombe haina faida kwake.
Tujiunge na Uwoya: “Mbali na kupoteza fedha nyingi lakini wakati mwingine nashindwa kutimiza ratiba yangu na hasa nikiwa na ‘apointimenti’ muhimu nashindwa kuitimiza kwa sababu ya pombe kwa hiyo natangaza rasmi kuacha na nawasihi wasanii wenzangu nao waache.”

Mwenyekiti Barclays ajiuzulu


 2 Julai, 2012 - Saa 03:42 GMT

Marcus Agius
Marcus Agius
Marcus Agius aliamua binafsi kujiuzulu kutokana kwa kile alichotaja katika taarifa yake ya kujiuzulu kama pigo kubwa linalotokana na kuharibiwa sifa kwa kampuni hiyo kwa sababu ya madai ya kuwalaghai wateja kupitia nyongeza haramu ya riba.
Wito umetolewa kuwa afisa mkuu mwandamizi wa kampuni hiyo, Bob Diamond ajiuzulu, kwa sababu alikuwa akisimamia uwekezaji wa benki hiyo wakati mpango ulipofanywa kulaghai wateja kupitia kwa riba inayotozwa katika benki hiyo.
Hata hivyo wakurugenzi wa Barclays wameamua kuwa Bwana Diamond ataendelea kufanya kazi.
Kwa hivyo Bwana Agius, ambaye pia ni mwanachama wa Bodi, aliamua, huku akiungwa mkono na wenzake, kujitwika lawama zote zinazotokana na madhambi yanayokabili Benki ya Barclays na hasira yote waliyo nayo wenye hisa wa benki hiyo.
Mtu anayetazamiwa kuchukua mahali pake ni mkurugenzi mwingine, Sir Mike Rake, ambaye kwa sasa atalazimika kujiuzulu vyeo vyake vya kuwa mwenyekiti wa Easyjet na BT.
Naye Bwana Diamond hajajiondoa katika lawama bado kwani atahojiwa na Wabunge kuhusu mawasiliano ya siri ya mwaka wa 2008 kati yake na naibu wa Gavana wa Benki Kuu, Paul Tucker.
Meneja wa Barclays wanaamini kuwa ni katika mawasiliano hayo ambapo Benki Kuu ya Uingereza iliamuru Benki hiyo kudanganya kuhusiana na riba inayotozwa.
Hiyo haikuwa kweli lakini Bwana Diamond atalazimika kuwaeleza Wabunge anachokumbuka Bwana Tucker akimweleza wakati ule na kile ambacho baadaye aliwaeleza wafanyakazi wenzake.
Itakuwa aibu kubwa kwao iwapo yeye au Bwana Tucker watagunguliwa kwamba waliwashawishi wenzao kulaghai kupitia riba haramu.

GARI LA WOLPER LAKAMATWA...


Jacqueline Wolper.

BMW X6 ya Wolper iliyokamatwa.
Wolper akishushwa kwenye gari lake.
Shakoor Jongo na Erick Evarist
LILE gari la kifahari aina ya BMW X6 lenye namba za usajili T 574 BXF linalomilikiwa na staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Masawe limedakwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa TRA ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, gari hilo la kisasa lilikamatwa Juni 28, 2012 kupitia Kampuni ya Mnada ya Majembe kutokana na sababu kadha wa kadha.
SABABU ZAANIKWA
Akiendelea kufunguka, afisa huyo alisema kuwa sababu ya kwanza ni kuhisiwa kuwa gari hilo liliingizwa nchini kinyemela kutokana na vielelezo vyake vya kwenye kadi kupitia kwenye vyombo vya habari, ndipo taa nyekundu ikawaka ndani ya vichwa vya maafisa wa TRA na kuanza kulifuatilia.
Alidai kuwa mbali ya kuingia nchini kinyemela, lakini BMW hilo halijalipiwa ushuru zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa mujibu wa vielelezo vyake.
MPANGO WA KULIKAMATA ULIVYOSUKWA
Kwa mujibu wa ofisa huyo, ili kufanikisha zoezi la kulikamata gari hilo, vijana kutoka kampuni ya Majembe waliingia mzigoni kulisaka ambapo kuna mtu alipiga kambi jirani na makazi ya Wolper, Mbezi Beach jijini Dar.
Ilisemekana kuwa vijana hao walikuwa na kazi moja tu, kuhakikisha anapotoka Jack wanamfuatilia hatua kwa hatua hadi mahali atakapokwenda kupiga kambi na kulitia mikononi.
“Haikuwa kazi rahisi maana muda mrefu alikuwa haonekani nalo, ndipo mpango huo ulipokuja kukamilishwa kwa njia ya kumfuatilia anapotoka kwake hadi mahali lilipokamatwa maeneo ya katikati ya Jiji la Dar,” alisema.
Akaendelea kudai: “Unajua hawa mastaa wetu kuna vitu wanavifanya bila kujua madhara yake, kitendo cha Wolper kuonesha kadi ya gari kwa waandishi wa habari huku anafahamu ina mapungufu kibao ndiyo sababu kuu ya gari hilo kuanza kufuatiliwa.”
MH! ETI USHURU MILIONI 70?
Taarifa nyingine ya kushtua ni kwamba ilidaiwa kuwa kuwa TRA peke yake inadai Sh. milioni 70 za ushuru.
“Si fedha ndogo zinazodaiwa na TRA, kwa hesabu ya harakaharaka ni zaidi ya Sh. milioni 70 ambazo zinatakiwa kulipwa.”
Baada ya The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda kujiridhisha kuwa gari hilo limedakwa, lilimuendea hewani Wolper lakini hakuweza kupokea simu hadi gazeti linakwenda mitamboni.