
Kasheshe iliyotokea juzi ndani ya klabu ya usiku yaNYC
Soho ya huko kwa Obama kati ya wasanii wawili wa nchini huko Drake na Chris
imeibua sakata jingine kwa mmiliki wa klabu hiyo ya usiku. Siku ya jumatano
kuliibuka ugomvi kati ya wakali hao ndani ya klabu hiyo huku kila mmoja akipewa
sapoti na wapambe wake ambapo Chris aliumizwa na Drake na kusababisha vurugu
kubwa ndani ya
klabu hiyo ambapo hapo baadae ilipelekea
mmiliki wa klabu hiyo kutafutwa na polisi kwa tukio hilo ambapo pia alikutwa na
makosa meningine baada ya kukamtwa. Jonathan Cantor mmiliki wa klabu hiyo
alikutwa na mkasa wa kukamatwa baada ya vurugu hizo zilitokea kwenye klabu yake
na sasa anakabiliwa pia na makosa ya kushindwa kudhibiti unywaji wa pombe na
kuwemo kwenye makosa mengine ya jinai.
No comments:
Post a Comment