9 Juni, 2012 - Saa 21:13 GMT
Timu ya Ureno ilionyesha haikuwa na mchezo wa kusisimua
Bao la Mario Gomez ambalo
lilifungwa kwa kichwa na katika dakika za mwishomwisho katika mechi ya
pili Jumamosi dhidi ya Ureno liliiwezesha Ujerumani kuondoka na ushindi
wa goli 1-0.
Tangu mwanzo ilionekana kwamba Ureno ilikuwa
katika hali nzuri ya kuitatiza timu ya Joachim Loew katika mechi hiyo
iliyochezewa uwanja wa Lviv.Ujerumani ilionekana kumiliki mpira kwa muda mrefu, lakini haikupata nafasi za moja kwa moja za kupata mabao.
Hata hivyo katika kipindi cha pili, Gomez alifanikiwa kufunga, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Sami Khedira, na kuianzishia Ujerumani kampeni safi ya Euro 2012 kwa ushindi huo.
Ureno walionekana kuwa hafifu, na waliamka mara tu baada ya Ujerumani kufunga, lakini ikawa vigumu kusawazisha.
Pepe aligonga mwamba, na baadaye hayo pia yakampata Nani, na ilielekea kweli ushindi ulikuwa ni wa Ujerumani.
No comments:
Post a Comment