Sunday, April 29, 2012

Mashariki mwa Congo hamkani tena

Ripoti kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinasema kuwa mapigano makali yametokea baina ya jeshi la serikali na askari watiifu kwa jenerali aliyeasi, Bosco Ntaganda.
Bosco Ntaganda
Inaarifiwa kuwa maelfu ya watu wamelikimbia eneo hilo katika majuma ya karibuni, tangu askari mia kadha wanaomuunga mkono Jenerali Ntaganda kuasi jeshini.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema, mvutano unaozidi mashariki mwa Congo ndio tatizo kubwa kabisa linalokabili baraza jipya la mawaziri, ambalo lilitangazwa jana.
Jenerali Ntaganda ni mpiganaji wa zamani, ambaye anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuwaajiri watoto kwenye jeshi lake.
Piya anasakwa na wakuu wa Congo.

No comments:

Post a Comment