Friday, April 27, 2012

Waandamana nusu uchi kulalamikia polisi

wanawake Uganda
Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.
Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.
Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.

Katibu Mkuu wa UN akemea hatua ya Sudan

Soko moja lilinyeshewa kwa mabomu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini.
Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.
Awali, Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE kujulikana mei 5 NDANI YA HOTELi YA KITALII YA NAURA SPRINGS


Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/= 

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo

Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S  ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.

No comments:

Post a Comment