Stori: Mwandishi Wetu
MELI ya MV Skagit imekwishazama kabisa kwenye Bahari ya Hindi eneo ambalo ilitokea ajali na zoezi la kutafuta maiti nyingine limesitishwa, serikali ilisema mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tamko hilo la serikali lilikuja huku ndugu wa watu ambao hawakupatikana wakiwa wanaumia kwa majonzi yasiyo na kifani kufuatia akili zao kushindwa kuamini kama kweli ndugu zao hawataonekana walikolala.
Baadhi ya watu waliozungumza na Ijumaa Wikienda, pia wameshangazwa na maajabu yanayotokana na kuzama kwa meli, vifo vya abiria na zoezi la uokoaji.
Wengi wanaamini kwamba ajali za meli huambatana na maajabu kwani haijawahi kutokea maiti wote kupatikana hata kama kukiwepo na wapiga mbizi maarufu wa dunia.
“Ajali ya MV Taitanic iliyozama miaka ya tisini, MV Bukoba mwaka 96, MV Spice Islanders, mwaka jana, MV Skagit na nyingine nyingi, abiria hawakupatikana wote. Ni lazima wengine wabaki,” alisema Maulid, mkazi wa Kariakoo, jijini Dar ambaye mke wa rafiki yake hakuonekana katika ajali hiyo.
Kikubwa walichosema wananchi baada ya serikali kutoa tamko hilo ni kwamba, inauma sana. Afadhali nduguyo afe umuone, umuhifadhi kaburini hata kama amekatika mikono yote kuliko kutomuona tena maisha.
Mpaka Jumamosi iliyopita, waliookolewa kwenye ajalio hiyo ni watu 146, maiti zilizoopolewa ni 68 huku watu wanaokadiriwa kufikia zaidi ya mia moja wakibaki ndani ya meli hiyo.
No comments:
Post a Comment