MNENGUAJI nyota wa bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma', Suzan
Godwin Chubwa 'Queen Suzy' hivi karibuni alipagawisha mashabiki katika
Manispaa ya Morogoro wakati wa hafla ya kumtafuta Miss Morogoro kutokana
na tatuu zake maridadi alizojichora mwilini.
Hafla hiyo ilifanyika Morogoro Hotel.
Akizungumza na mtandao huu, mrembo huyo ambaye kabla ya kujiunga na
bendi hiyo alikuwa na bendi ya African Stars wajulikanao kama ‘Twanga
Pepeta’, alisema mapambo hayo ni kwa ajili ya kuwachengua mashabiki
wake wakati akinengua jukwaani.
No comments:
Post a Comment