29 Agosti, 2012 - Saa 10:32 GMT
Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema kuwa serikali yake inahitaji muda wa ziada kuweza kushinda vita dhidi ya waasi nchini humo.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni kinachounga mkono serikali ya Assad,rais huyo pia alipuuza tamko kuwa haiwezekani kutenga maeneo ya kutolea misaada katika maeneo ya mipaka nchini humo,
Wanaharakati wa upinzani wanadai kuwa jeshi limefanya mashambulizi katika maeneo mengi ya nchi hiyo kutaka kudhibiti maeneo yaliyotekwa na waasi.
Mapambano makali yaliripotiwa kutokea siku ya Jumanne katika mji mkuu Damascus, Aleppo na mkoa wa kaskazini masharibi wa Idlib.
Bwana Assad amesema kuwa serikali yake iko kwenye vita ndani na nje ya nchi.
"bila shaka tunahitaji muda zaidi kuweza kumaliza vita hivi katika njia inayofaa. Lakini ninachoweza kusema ka neno moja tu ni tunapiga hatua''. Bwana Assad alisema.
"hali kwa sasa angalau ni nzuri, lakini bado hatujafika mwisho. Hilo bila shaka linahitaji muda zaidi'' alisema Assad
''Maafisa wa ulinzi wanafanya kitendo ha ushujaa kwa kila hali. Lakini waasi hawataruhusiwa kueleza hofu wala hawataruhusiwa kiufanya hivyo.'' aliongeza rais Assad.
Kila mtu hapa nchini ana wasiwasi kuhusu hali ya nchi yetu, hilo ni jambo la kawaida.Ninawaambia wananchi wa Syria, mustakabali a nchi hii uko mikononi mwenu, wala sio mikononi mwa watu wengine''.
Rais aliwakejeli maafisa wakuu wa serikali na jeshi ambao wameasi serikali katika miezi ya hivi karibuni akisema kuwa hatua hiyo iliweza kuisafi serikali mwanzo na kisha nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment