Friday, August 24, 2012
Mmoja wa wasanii mahiri
katika fani ya uigizaji hapa nchini, Wema Sepetu akifanya mahojiano
mafupi na Millard Ayo wa Clouds FM mapema leo kwenye amsha amsha ya
tamasha la Serengeti Fiesta ambalo linafanyika jioni ya leo mpaka lyamba
ndani ya uwanja wa chuo cha Ushirika, ndani ya mji wa Moshi,ambapo
katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni nusu mnyama tu a.k.a
5,000/= kwa kila kichwa. Wema
Sepetu pia aalisema ujio wao ndani ya mji wa Moshi,kuwa wao kama
Wasanii Nyota wa Filamu wamewasili mkoani humo kusaka vipaji vipya
mbalimbali vya filamu,usahili huo unafanyika kwenye ukumbi wa Mr
Price,ulioko mtaa wa Malindi.
Mtangazaji wa Clouds FM,Millard
Ayo akiwa Live mapema leo mtaa wa Malindi katika mpango mzima wa amsha
amsha kwa wakazi wa Moshi kuhusiana na tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo
pia katika tamasha hilo kutatolewa zawadi mbalimbali ikiwemo gari ndogo
aina ya Vits kama uinavyo pichani ikinadiwa vilivyo.
Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka kampuni ya Gapco ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.
Kawa kawa amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta pia linatoa mafuta kwa magari daladala,pikipiki sambamba na baji lita 10 ama tano kutoka kampuni ya Gapco ambao pia ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo.
Msanii mwingine nyota katika tasnia
ya filamu,Aunt Ezekiel akielezea ni namna tamasha la Serengeti Fiesta
lilivyowambamba wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake,na pia ujio
wao kuwatafuta wasanii wapya chipukizi katika tasnia hiyo ambayo imekuwa
ikikua siku hadi siku.
Wema Sepetu katika pozi na washabiki wake mapema mchana huu.
Mastaa wetu wa filamu hapa nchini, wametokelezeaje sasaaa.
Kiongozi wa msafara wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mully B akiwa na mastaa wa filamu,Wema Sepetu na Aunt Ezekiel afu fulllll BBM kama kawa.
Millard Ayo akifanya mahojiano na Ray a.k.a Vincent Kigosi kuhusiana na ujio wao ndani ya mji wa Moshi
Kutoka kushoto ni Mr Hatman,Steve Nyerere,Bonge pamoja na Millard Ayo katika shoo love ya pamoja.
Wakiwa katika mazungumzo yao ya hapa na pale.
Kila mmoja ana haki ya kupata habari na kuhabarishwa.
Pichani ni Gari aina ya Vits itakayotolewa jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,kwa
mshindi atakaejishindia kwenye droo itakayofanyika katika uwanja wa
chuo cha ushirika,ambako tamasha hilo litarindima mpaka majogoo.
Jacob Steven a.k.a Steven akifafanua
jambo mapema leo mtaa wa Malindi kuhusiana na suala zima la wasanii hao
kulivamia jiji la Moshi
No comments:
Post a Comment