Serikali ya Tanzania inasema
meli za mafuta 36 za Iran zimesajiliwa tena nchini Tanzania, ili
kujaribu kuhepa vikwazo dhidi ya Iran vilivowekwa na Marekani na Umoja
wa Ulaya.
Mafuta ya Iran yamewekewa vikwazo, ili kuishawishi Iran iache mradi wake wa nuklia.
Tanzania imeacha kuagiza mafuta kutoka Iran.
Uchunguzi ulifanywa na serikali ya Tanzania, baada ya mbunge mmoja wa Marekani, Howard Berman, mwenyekiti wa kamati ya Congress ya maswala ya nchi za nje, kueleza wasiwasi wake juu ya meli hizo za Iran kupatiwa bendera ya Tanzania.
Tanzania sasa inasema itafuta usajili wa meli hizo.
No comments:
Post a Comment