SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Anna Makinda,
juzi Jumatatu msafara wake ulinusurika risasi na mabomu ya machozi ya
polisi wa Morogoro waliyokuwa wameyalenga kwa wafuasi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) eneo la Msamvu, barabara kuu ya
Morogoro-Dar es Salaam. Mwandishi wetu alimshuhudia spika akitokea
lringa kwa gari na kupita eneo la Msamvu ambapo muda mfupi baadaye
polisi walianza kurusha mabomu ya machozi na risasi na kumwua kijana
Ally Zolla na vijana wengine wawili kujeruhiwa.
(NA DUNSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
(NA DUNSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
No comments:
Post a Comment