Hamida Hassan na Gladness Mallya
BAADHI ya mastaa Bongo wanadaiwa kuwa na tabia ya kutumia mtandao wa
simu wa BlackBerry Messenger ‘BBM’ vibaya ikiwa ni pamoja na kujiuza kwa
wanaume, Ijumaa limebaini.
Utafiti uliofanywa na mapaparazi wetu
umeonesha kuwa, wapo ambao wawapo vyumbani kwao hujipiga picha za utupu
na kuzitupia kwenye mtandao huo kisha baada ya muda huzitoa.
Wakizungumzia tabia hiyo, baadhi ya wanaume wanaotumia BBM walikiri
kukumbana na picha hizo za ajabu za mastaa huku zikiambatana na maneno
ya kujitongozesha kwao.
“Huyu …(anataja jina la staa maarufu Bongo),
juzi usiku mishale ya saa nane alianza kunitumia ‘sms’ kuniuliza kama
niko macho. Nilipomjibu akaniambia kuna zawadi anataka kunipa,
nilivyomkubalia akatupia picha yake akiwa kitandani mtupu.
“Hazikupita hata sekunde nyingi, kabla ‘sijai-download’ akaitoa kisha
akaniuliza nimejisikiaje kumuona alivyo. Nilishangaa lakini nikamjibu
kwa kifupi kuwa ana mvuto, basi kuanzia siku hiyo akawa ameniganda,”
anasema kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sule ambaye ni
mfanyabiashara jijini Dar.
Msanii mwingine wa kiume aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
“Mbona huo ndiyo mchezo wao, yaani ukishamkubalia kuwa rafiki yao basi
subiri vituko, kwa kifupi sasa hivi wengi wanajiuza kupitia BBM.”
Katika kupata ukweli juu ya habari hiyo, waandishi wetu walizungumza na
baadhi ya mastaa wa Kibongo wanaotumia mtandao huo ambapo walikuwa na
haya ya kusema:
JACQUELINE PATRICK
Modo huyo mwenye jina
kubwa Bongo alifunguka: “Kwa upande wangu siwezi kukataa kuwa sijawahi
kuweka picha kama hizo, mimi ni mpenzi sana wa picha na ninaupenda sana
mwili wangu hivyo nikipiga picha ya aina yoyote lazima niitupie kwani
‘fansi’ wangu ndiyo wanaoweza kuniambia kama nimenenepa au nimekonda au
kunisifia.
“Suala la kutongoza wanaume naweza nikasema kuwa mimi
siweki kwa sababu hiyo kwani marafiki zangu wote kwenye BBM wana wapenzi
wao.”
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Mwigizaji huyo ambaye pia
ni mwanamuziki alisema: “Mimi sijawahi kumtongoza mwanaume na siwezi kwa
sababu mila za kwetu zinasema mwanaume ndiye anatakiwa kumtongoza
mwanamke hivyo mwanamke anayemtongoza mwanaume anakosea kwani ataonekana
wa bei rahisi sana.
Labda wenzangu wanaweza kufanya hivyo kupitia njia hiyo.”
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Mwigizaji huyo alifunguka: “Mimi nina mume wangu, nampenda sana na mara
nyingi siingii BBM ila ninauzisha tu picha zangu kule lakini kuchati na
watu siyo kivile na siwezi kumtongoza mwanaume kwa sababu wanaume
wanaopatikana kwa njia hiyo siyo kabisa labda mastaa wenzangu, lakini
mimi sijawahi kumtongoza mwanaume.”
RACHEL HAULE ‘RECHO’
Staa huyo wa filamu alisema: “Sijawahi kumtongoza mwanaume ila suala la
kutongozwa na wanaume kwenye BBM ni la kawaida, inategemea na msimamo wa
mtu. Najua BBM tumejiunga kwa ajili ya kujua matukio yanayotokea kwa
haraka zaidi na siyo kwa ajili ya kujiuza.”
ISABELA MPANDA
Mwigizaji huyo alitiririka: “Katika orodha ya hao wanaojiuza kupitia
mtandano huo, mimi simo. Nipo BBM ila sijawahi kumtongoza mtu wala
kutupia za utupu.”
RUTH SUKA ‘MAINDA’
Mwigizaji huyo mkongwe alisema: “Ni kweli nimejiunga BBM lakini kwa sasa nipo ‘shouting’ nicheki baadaye.
Mastaa wengine waliotajwa kuwepo BBM nja na waigizaji Aunt Ezekiel, Irene Uwoya, Agnes Gerard ‘Masogange’ na wengineo.
No comments:
Post a Comment