Monday, April 30, 2012

Historia ya Charles Taylor

Charles

Charles Taylor amekutwa na hatia
Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imempata na hatia aliyekua Rais wa Liberia, Charles Taylor, kwa kosa la kushiriki na kusaidia uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji, ubakaji na ugaidi.
Mahakama ya huko The Hague imesema kua Bw Taylor anawajibika kwa kuunga mkono waasi wa kundi lililojulikana kama RUF yaani Revolutionary United Front katika nchi jirani ya Sierra Leone wakati wa vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka 1990.

Bw Taylor ndiye kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukabiliwa na hukumu mbele ya Mahakama ya Kimataifa tangu kesi maarufu za Nuremburg baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia. Atahukumiwa mwezi ujao.
Maelezo yafuatayo yalikusanywa na kuandikwa na mwandishi wa BBC aliye nchini Liberia na mara kadhaa alikutana na Charles Taylor.
Charles Taylor alikua Rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi alipojiuzulu mnamo mwaka 2003 kufuatia shinikizo kali za kimataifa. Alianza shughuli za siasa wakati wa ziara yake nchini Liberia kama kiongozi wa msafara wa mashirika ya Waliberia yaliyo barani Amerika mapema katika muongo wa 1980, mapinduzi ya kijeshi yalipofanyika naye kupewa kazi katika serikali ya Samuel Doe.
Baada ya kuteuliwa kama Naibu waziri katika Wizara ya biashara ya serikali ya Rais Doe, Taylor aliikimbilia Marekani kufuatia madai kwamba amepoteza takriban dola za kimarekani milioni moja.
Alifungwa huko Marekani lakini akatoroka jela katika mazingira ambayo hadi leo bado ni ya kutatanisha. Hatimaye aliunda kundi lake la waasi, lililojulikana kama National Patriotic Front of Liberia, ambalo liliiondoa serikali ya Samuel Doe madarakani.
Taylor
Alikuwa kiongozi wa waasi
Taylor ana kipaji cha kua mtu mchangamfu ambaye aliweza kumbadili adui na kumpenda kiasi cha kumfanya kua mfuasi sugu. Kwa mfano alipoingia mji wa Monrovia mnamo mwaka 1995 makumi kwa mamia ya watu waliompinga walijitokeza kumpokea na kumuimbia nyimbo za kumsifu kama shujaa.
Licha ya kuwateua watu wengi kama washauri wake lakini hiyo ilikua danganya toto'' kwa sababu hakufuata ushauri wao hata siku moja. Mmoja wa washauri wake wa karibu aliwahi kuniambia kua yaliyomfika Taylor yangeweza kuepukika kama angewasikiliza washauri hao.
Taylor alipenda sana kujifananisha na watawala wa enzi ya karne ya kumi na tisa kwa jinsi alivyowazawadia fukara akifahamu kua fadhila zake zitamjengea sifa na kumfaa siku moja.
Akiwa mpenda madaha alifahami vyema nguvu ya vyombo vya habari na jinsi ya kuvitumilia. Kupitia miaka ya 1990 alishiriki mahijiano mengi ya kipindi cha BBC cha Focus on Africa.
Katika kipindi cha kwanza, akiwa ni kiongozi wa kundi la waasi asiyefahamika, alitangaza mpango wake wa kuivamia Liberia.
Miaka michache baadaye, alipodokezewa na mtangazaji kwamba watu wengi wanamuonelea kua muuwaji, alilipuka na kusema ''Hata Yesu Kristu alituhumiwa kua ni muuwaji enzi zake.
Katika mahojiano mengi tuliyofanya naye daima alijitahidi kudhibiti mahojiano ili kutoa sura inayompendeza yeye. Mfano uilipomrushia suali lililomchukiza alijitahidi kulibadili liweze kusikika kwa manufaa yake.
Kama mpiganaji mahiri alijivunia uwezo wake wa kiume na uwezo wa kuzaa watoto wengi. Hakuficha siri yake ya kupenda wanawake, akidokeza wakati mmoja kua kama kiongozi wa Kiafrika ana haki ya hadi wake wanne.
Naomi
Mwanamitindo Naomi Campbell alihusishwa katika kesi ya Taylor
Wakosoaji wake walipokashifu tabia yake ya uzinzi, alijibu kwa kuwakemea wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na kujibu ''Bora mimi nawapenda wanawake.''
Mnamo mwaka 1996 alidokezea kua angetaka kujaliwa na watoto wengine watano na wote watakua wanaume. Hata hivyo hakujaliwa na ndoto yake hio watoto wake wawili waliofuata walikua wa kike.
Labda kama ishara ya kujiliwaza majaliwa hayo, aliwahi kuniambia kua kama mzazi anayewapenda wanawe, mume yeyote atakayewaoa wanangu, itabidi akubali watoto wake warithi jina la Taylor liendelee kudumu katika familia

Sunday, April 29, 2012

Rahman next on Povetkin’s way toward Klitschko bout


U.S. heavy weight boxer Hasim Rahman. (Reuters / Kai Pfaffenbach)
U.S. heavy weight boxer Hasim Rahman. (Reuters / Kai Pfaffenbach)
TAGS: Boxing, Povetkin

After a great uncompromising battle between Aleksandr Povetkin and Marco Huck, and the Russian’s hard victory on points, fans are demanding an immediate rematch. However, the fight will not happen - at least for now.
WBA regular champion Povetkin (24-0, 16 KOs) retained his title with a very tough majority decision over WBO cruiserweight king Marco Huck (34-2, 25 KOs). The scores (114-114, 116-113 and 116-112) are being called controversial by some observers, who saw Huck as the winner.
In a post-fight televised interview, Povetkin said he was ready for a rematch. But according to Chris Meyer, CEO for Sauerland Event, the Russian is now obliged to hold a mandatory defense against former WBC champion Hasim Rahman (50-7-2, 41KOs).
"Povetkin has to do his mandatory against Hasim Rahman first. We can't get around it," Meyer told boxingscene.com.
In case the Russian Knight beats the American veteran, he will be able to challenge WBA, WBO and IBF champion Wladimir Klitschko.
As for WBO cruiserweight king Huck, he has now to decide whether to return to cruiser or remain at heavyweight.

Gaddafi put up 50M euro for Sarkozy’s presidential bid – report


France's President and UMP party candidate for the 2012 French presidential elections, Nicolas Sarkozy (Reuters / Philippe Wojazer)

France's President and UMP party candidate for the 2012 French presidential elections, Nicolas Sarkozy (Reuters / Philippe Wojazer)

Former Libyan leader Muammar Gaddafi had agreed to fund French President Nicolas Sarkozy’s 2007 election campaign – to the tune of 50 million euro, a new report says.
The Paris-based investigative website Mediapart published “documentary evidence” that Gaddafi was ready to stump up tens of millions of dollars to help Sarkozy win the French presidential race.
Mediapart claimed Saturday that the 2006 document was provided by "former senior [Libyan] officials, who are now in hiding."  They further claim the document came “from the archives of the secret service,” and was signed by Gaddafi’s former intelligence chief and later foreign minister, Moussa Koussa.
In it, Koussa noted “an agreement in principle to support the campaign for the candidate for presidential election, Nicolas Sarkozy, for a sum equivalent to 50 million euro."
Sarkozy attempted to deflect the allegations when confronted by a TF1 presenter, saying, "If [Gaddafi] had financed it, I wasn't very grateful." Sarkozy’s sarcastic comeback was in reference to France’s lead role in the NATO campaign that led to Gaddafi’s brutal demise.
'It's obviously an attempt to draw away attention after Dominique Strauss-Kahn is back on stage,' Nicolas Sarkozy told the French media.
On Friday the former IMF-chief, who was once tipped to win France's presidential vote, but dropped out of the race after a sex scandal, claimed Sarkozy and other political rivals orchestrated his downfall.
'This only plays into Socialists' hands as they don't want to be reminded that they were going to make him the next French president,' Sarkozy added.
It’s not the first time the French president denies allegations his 2007 campaign was sponsored by Tripoli.
In March 2012 Sarkozy also rejected claims he took €50 million from Muammar Gaddafi.
The scandal with alleged finance from Libya dates back to March 2011 when Gaddafi's son Saif al-Islam demanded that Sarkozy return the money his family had given for the 2007 campaign:
 “He's disappointed us. We have all the bank details and documents for the transfer operations and we will make everything public soon," – threatened Saif al-Islam in a TV interview during the NATO-backed military campaign in Libya.
French politicians are banned from receiving campaign contributions from foreign states, and a French judge is currently looking into the allegations.
The latest document has surfaced at a particularly sensitive time for Sarkozy, who lost the first round of the French presidential vote and is currently trailing his Socialist rival Francois Hollande in the polls.

Newcastle yaangukia pua yalazwa 4-0

Wigan imeendelea kuonesha kandanda maridadi baada ya kuillaza Newcastle mabao 4-0 na kudhihirisha nia ya kujinusuru kuteremka daraja, matokeo ambayo pia yameivurugia Newcastle nafasi ya kuikalia nafasi ya tatu hatimaye kucheza moja kwa moja Ligi ya Ulaya msimu ujao.

Victor Moses shujaa wa Wigan
Victor Moses shujaa wa Wigan
Victor Moses alikuwa wa kwanza kuipatia mabao Wigan akifunga mabao mawili katika muda wa dakika mbili na kumuweka katika hali mbaya Tim Krul mlinda mlango wa Newcastle.
Shaun Maloney akaongeza bao la tatu na kujihakikishia ushindi kabla ya Franco di Santo kushindilia msumari wa mwisho kabla ya mapumziko na ubao wa mabao ukasomeka Wigan 4 Newcastle 0.
Papiss Cisse ambaye tangu ajiunge na Newcastle amekuwa akipachika mabao karibu kila mchezo, mkwaju wake uligonga mwamba lakini hata hivyo timu hiyo ilionekana wanyonge kwa Wigan na kuziachia pointi tatu muhimu.
Huu ni ushindi wa tano wa Wigan katika mechi sita zilizopita na kusogea pointi tatu mbele kutoka eneo la hatari la kuteremka daraja wakisaliwa na mechi mbili kabla hawajamaliza msimu.
Arsenal ilisogea karibu kuishika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kulazimishwa sare na Stoke.
The Gunners walianza kufungwa baada ya Peter Crouch kuunganisha kwa kichwa mpira wa juu uliopigwa pembeni na Matthew Etherington.
Arsenal haraka wakajibu shambulio wakati Tomas Rosicky pasi yake ya pembeni ilipounganishwa wavuni na Robin van Persie.
Yossi Benayoun alinyimwa mkwaju wa penalti baada ya Glenn Whelan kumuangusha ndani ya eneo la hatari wakati muda ukiwa umeyoyoma na timu zote zikiwa zimeridhika kwa kugawana pointi moja moja.
Nikica Jelavic aliifungia Everton mabao mawili ikiwa ni hatua moja mbele juu ya Liverpool wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa kupendeza wa mabao 4-0 dhidi ya Fulham katika uwanja wa Goodison Park.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Croatia alifunga mabao yake hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kabla ya mapumziko Marouane Fellaini aliongeza bao la tatu.
Tim Cahill aliyeingia kipindi cha pili aliiongezea Everton bao la nne, wakati Fulham wakiwa wamekwisha sambaratika.
Ushindi huo umeinyanyua Everton hadi nafasi ya saba, wakiwa pointi tano zaidi ya Fulham.
Everton wanamaliza msimu kwa kishindo huku meneja wao David Moyes akiwa na nia ya kukamata nafasi nane bora za juu baada ya muda wa miaka 11.
Everton haijawahi kumaliza juu ya Liverpool katika msimamo wa Ligi Kuu ya England tangu mwaka 2005, lakini huu ni msimu wao wa tatu wenye manufaa.
Kevin Davies alifunga mabao mawili na kuipatia pointi moja Bolton wakati Sunderland iliposhindwa kuendeleza wimbi la ushindi kwa mchezo wa tano.
Nahodha huyo wa Bolton alijaza mpira wa juu wavuni kufuatia pasi ya pembeni ya Martin Petrov kabla Nicklas Bendtner kuisawazishia Sunderland.
Mkwaju wa James McClean wa adhabu ya moja kwa moja uliipatia Sunderland bao la pili kabla Davies tena hajaiokoa Bolton kwa kusawazisha na kuionesha Sunderland kwa nini walitaka kumsajili mwezi wa Januari.
Nayo Aston Villa iliambulia pointi moja baada ya kuilazimisha West Brom kutoka sare ya kutofungana.
Villa walipata nafasi nzuri kipindi cha kwanza, wakati Gabriel Agbonlahor mara mbili mikwaju yake ilipookolewa na mlinda mlango wa West Brom Ben Foster.
Lakini wenyeji walinyimwa mkwaju wa penalti baada ya mapumziko wakati Alan Hutton alipozuia mpira wa kichwa uliopigwa na Liam Ridgewell na kumgonga mkononi na kupaa juu ya lango.
Timu zote mbili zilipata nafasi nzuri wakati mpira ukielekea kumalizika.
Mabao mawili ya Matt Jarvis yaliiwezesha Wolves kupigana kiume na kuilazimisha Swansea kutoka nayo sare ya mabao 4-4 katika pambano zuri na la kusisimua.
Pambano hilo lililoanza kwa kasi tangu mwanzo lilishuhudia Andrea Orlandi na Nathan Dyer wakipachika mabao ya haraka haraka Swansea.
Steven Fletcher wa Wolves aliuchepua kwa kichwa na kufunga bao la kwanza akijibu shambulio la Swansea kabla ya mpira wa pembeni wa Danny Graham kujaa wavuni na ubao wa mabao ukasomeka 4-1. Baadae Jarvis akafanikiwa kuweka wavuni mabao mawili na kuikoa Wolves kwa kipigo kingine.
Wolves waliingia uwanja wa Liberty Stadium wakiwa mkiani mwa msimamo wa ligi na tayari wameshateremka daraja na dalili za awali zilionesha watashindiliwa kucheza ligi ya Championship kwa kuvurumishiwa mabao mengi hali ambayo ikawa tofauti

Chambers atakimbia London 2012

Dwain Chambers
Mwanariadha wa mbio fupi wa Uingereza Dwain Chambers sasa anaruhusiwa kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya London 2012
Dwain Chambers sasa anaweza kushiriki katika mashindano ya London 2012, kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya rufaa inayohusika na michezo duniani, Court of Arbitration for Sport (Cas).
Chama cha Olimpiki cha Uingereza, BOA, kimekuwa na sera ya kuwazuia maisha wanariadha wanaoadhibiwa kwa kutumia dawa za kuongezea nguvu michezoni kutoshiriki katika mashindano.
Chama hicho cha Olimpiki kimeshindwa kuitetea sera hiyo iliyopingwa na chama cha dunia cha kupambana na dawa za kuongezea nguvu michezoni (World Anti-Doping Agnecy), kwa kifupi Wada, mzozo ambao ulifikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa inayohusika na michezo,
Uamuzi wa mahakama hiyo unamaanisha kwamba Dwain Chambers, mwenye umri wa miaka 34, na mweneshaji baiskeli David Millar, mwenye umri wa miaka 35, wote kama Waingereza, wanaweza kufuzu kujiunga na timu ya taifa, maarufu kwa jina Team GB.
Mahakama ya kimataifa ya kesi za michezo inatazamiwa rasmi kutangaza uamuzi wake Jumatatu, saa kumi na moja alasiri.
Hata hivyo wanariadha watawajibika kufuzu katika mashindano ili kufikiriwa kama itawezekana kujiunga na timu ya taifa.
Wanamichezo wa Uingereza ambao daima dawama wamekatazwa na chama cha Olimpiki cha Uingereza kushiriki katika mashindano ya Olimpiki katika maisha yao yote ni Dwain Chambers, David Millar, Carl Myerscough, Peter Meakin, Jade Mellor, Callum Priestley, Dan Staite na Jamie Stevenson.
Chambers aligunduliwa kutumia dawa aina ya THG mwaka 2003, na aliadhibiwa asishiriki katika mashindano ya riadha kwa miaka 2, na mwaka mmoja baadaye, Miller naye alipewa adhabu hiyohiyo, baada ya kukiri kutumia dawa ya kuongezea damu nguvu ya EPO.
Wanariadha wote wawili tangu wakati huo wameshirikiana na maafisa mbalimbali wa kupambana na kuzuia utumizi wa dawa za kuongezea nguvu michezoni.
Chama cha Olimpiki cha Uingereza kimekuwa kikijitetea kwamba kina haki ya kuamua kuwazuia maisha Waingereza wanaogunduliwa kutumia dawa za kuongezea nguvu, hata baada ya wanamichezo hao kukamilisha adhabu waliopewa, jambo ambalo limekuwa likipingwa na Wada.
Wakuu wa chama cha Olimpiki cha Uingereza waliifikisha kesi hiyo mahakamani kupinga msimamo wa Wada.
Wada ilikuwa imesema sera ya chama cha Olimpiki cha Uingereza haiambatani na kanuni za Wada.
Sheria hiyo ya chama cha Olimpiki cha Uingereza, ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka 20, imewazuia wanamichezo wengi kushiriki katika mashindano ya Olimpiki yaliyopita.

Torres afunga matatu, Blackburn hatarini

Fernando Torres amepachika mabao matatu murua na kuweka hai matumaini ya Chelsea kumaliza katika nafasi nne za juu za msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England, walipoilaza QPR mabao 6-1 ambao wapo hatarini kushuka daraja.
Fernando Torres akishangilia moja ya mabao yake akiwa na John Terry
Fernando Torres akishangilia moja ya mabao yake akiwa na John Terry
Daniel Sturridge alikuwa wa kwanza kufungua karamu ya mabao mapema tu sekunde ya 45 na baadae John Terry akapachika bao la pili kwa kichwa akifuatiwa na Torres aliyeweka wavuni mabao mawili ya haraka haraka na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa mabao 4-0 hadi dakika 25 kipindi cha kwanza.
Torres alikamilisha mabao yake matatu baada ya mapumziko na Florent Malouda akafunga kitabu kwa kuandika bao la sita kabla ya Djibril Cisse kuipatia QPR bao moja la kufutia machozi.
Matokeo hayo yameibakisha Chelsea katika nafasi ya sita huku QPR ikiwa juu ya mstari wa kuteremka daraja kwa tofauti ya mabao na Bolton.
Katika mchezo mwengine Tottenham imefanikiwa kujiinua hadi nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya Kandanda ya England baada ya kuilaza Blackburn mabao 2-0. Blackburn wana wasiwasi mkubwa wa kuteremka daraja msimu huu na kufungwa kwao kumewazidishia hofu hiyo.
Rafael van der Vaart alitangulia kuipatia Spurs bao la kwanza kwa kwaju wa karibu baada ya mpira wa kichwa uliopigwa na Gareth Bale kugonga mwamba wa lango la Blackburn.
Kyle Walker akiwa umbali wa yadi 25 aliachia mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja na mpira ukaenda moja kwa moja wavuni na kuipatia Spurs bao la pili dhidi ya Rovers ambao wapo nafasi ya pili kutoka mkiani na hawakuonesha mchezo wowote wenye nia ya ushindi.

Mashariki mwa Congo hamkani tena

Ripoti kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinasema kuwa mapigano makali yametokea baina ya jeshi la serikali na askari watiifu kwa jenerali aliyeasi, Bosco Ntaganda.
Bosco Ntaganda
Inaarifiwa kuwa maelfu ya watu wamelikimbia eneo hilo katika majuma ya karibuni, tangu askari mia kadha wanaomuunga mkono Jenerali Ntaganda kuasi jeshini.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema, mvutano unaozidi mashariki mwa Congo ndio tatizo kubwa kabisa linalokabili baraza jipya la mawaziri, ambalo lilitangazwa jana.
Jenerali Ntaganda ni mpiganaji wa zamani, ambaye anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuwaajiri watoto kwenye jeshi lake.
Piya anasakwa na wakuu wa Congo.

Sudan yawataka raia wa Kusini waondoke

Rais wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini
Serikali ya Sudan imesema zaidi ya raia wa Sudan kusini 12,000 wanapaswa kuondoka nchini humo katika kipindi cha wiki moja.
Gavana wa jimbo la White Nile,Yusuf -shabali, amesema kuwepo kwa raia hao katika eneo la Sudan kunasababisha tisho la usalama na la kimazingira.
Amewapatia raia hao wa kusini muda wa wiki moja kuondoka.
Sudan na Sudan kusini zimekuwa zikizozania eneo la mpaka baina ya nchi hizo, lenye utajiri wa mafuta wiki kadhaa za hivi karibuni.
Bwana Al-Shambali amesema serikali ya Sudan Kusini ilikubali kuwahamisha raia wake, zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Wengi wa raia hao wa kusini walihamia Kaskazini punde baada ya mkataba wa mwaka wa 2002, ili kutafuta ajira.
Maelfu ya raia hao kwa sasa wako jiani kuelekea nyumbani, lakini wamekwama katika mto wa Port Kosti karibu na mpaka na Sudan Kusini.
Serikali ya Khartoum imekataa kuwapa kibali cha kuiwezesha serikali ya Sudan Kusini iwavukisha ili waweze kuingia nchini mwao.
Serikali ya Sudan imekataa kuwapa kibali cha kurudi hadi ipate hakikisho kutoka kwa Sudan Kusini kuwa haitatumia vibali hivyo kupitisha vifaa vya kijeshi na wapiganaji nchini Sudan.

Waziri wa zamani wa Libya afariki

Waziri wa mafuta wa zamani wa Libya amekutikana amekufa katika mji mkuu wa Austria, Vienna, karibu na mto Danube, kwa mujibu wa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje ya Austria.
Shukri Ghanem
Shukri Ghanem, aliyekuwa na umri wa miaka 69, alikuwa mmoja kati ya wakuu maarufu waliokimbia kutoka serikali ya Kanali Gaddafi wakati wa ghasia za Libya.
Hakujatolewa maelezo zaidi, lakini inafikiriwa amekufa kutokana na ugonjwa wa moyo.
Inafikiriwa amekuwa akiishi Ulaya tangu mwezi Juni mwaka jana.

Mripuko kwenye kanisa mjini Nairobi, Kenya, umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine 10.


Polisi wanasema guruneti lilirushwa kwenye kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, wakati wa ibada ya asubuhi.

Daktari mmoja katika Guru Nanak Hospital mjini Nairobi, ambako ndiko majeruhi walikopelekwa, aliwaelezea waandishi wa habari majeruhi aliowaona:

"Tumepokea majeruhi 7, mwanamke mmoja aliumia vibaya kwenye mguu wa kushoto, ambao umevunjika mahala kadha.

Mwanamme mmoja alikuwa na majaraha kadha kwenye nyama na tunafikiri amevunja mifupa piya; labda tukimfanyia x-ray tutatambua.

Kuna mama mmoja aliyevunja kidogo kisuguru cha mguu wa kushoto, na wengineo wamepata mikwaruzo-kwaruzo na kujikata-kata."

Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.

Saudi Arabia yafunga ubalozi Misri


Saudi Arabia imemrudisha nyumbani balozi wake nchini Misri na imesema imefunga ofisi zake zote huko, baada ya maandamano ya hasira kulalamika juu ya wakili wa Misri wa kugombea haki za kibinaadamu kukamatwa na wakuu wa Saudi Arabia.


Ahmed El-Gizawy alikamatwa awali mwezi huu alipowasili Saudi Arabia kwa hija.

Wasaudi wanasema alijaribu kuingiza kwa magendo vitu vinavokatazwa, lakini wanaharakati wanasema el-Gizawy alikamatwa kwa sababu aliwahi kupeleka malalamiko juu ya namna wafungwa kutoka Misri wanavotendewa nchini Saudi Arabia.

Mapema juma hili, mamia ya watu waliandamana nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Cairo kudai wafungwa hao waachiliwe huru haraka.

CIARA BLOG: Afisa hataki Israil ishambulie I...

CIARA BLOG: Afisa hataki Israil ishambulie I...: Afisa hataki Israil ishambulie Iran Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasu...


Saudi Arabia yafunga ubalozi Misri

 


Saudi Arabia imemrudisha nyumbani balozi wake nchini Misri na imesema imefunga ofisi zake zote huko, baada ya maandamano ya hasira kulalamika juu ya wakili wa Misri wa kugombea haki za kibinaadamu kukamatwa na wakuu wa Saudi Arabia.



Ahmed El-Gizawy alikamatwa awali mwezi huu alipowasili Saudi Arabia kwa hija.


Wasaudi wanasema alijaribu kuingiza kwa magendo vitu vinavokatazwa, lakini wanaharakati wanasema el-Gizawy alikamatwa kwa sababu aliwahi kupeleka malalamiko juu ya namna wafungwa kutoka Misri wanavotendewa nchini Saudi Arabia.


Mapema juma hili, mamia ya watu waliandamana nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Cairo kudai wafungwa hao waachiliwe huru haraka.

 


Mlipuko waua watu 70 Hama Syria

 


Watu takriban 70 wameuawa katika shambulio kwenye nyumba moja katika eneo la Hama, hayo ni kwa mujibu wa wanahakarakati wa Syria.


Wanasema nyumba kadhaa katika wilaya ya Masha at-Tayyar kusini mwa Hama ziliharibiwa kutokana na shambulio kubwa.


Shirika la habari la serikali linasema kuwa watu 16 waliuawa ndani ya nyumba iliyokuwa ikitumiwa kama kiwanda cha kutengeneza mabomu na "kundi la magaidi".


Makabiliano hayo yametokea licha ya Umoja wa Mataifa kutaka mapigano yasitishwe - ikiwa ni mpango wa amani uliopendekezwa na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kiarabu Kofi Annan.

Sudan Kusini yapata mkopo mkubwa Uchina


Sudan Kusini inasema kuwa imepewa mkopo na Uchina wa dola bilioni 8, kugharimia miradi kadha ya miundo mbinu.

Taarifa zinazohusiana
Sudan Kusini,
Siasa

Ikiwa utatekelezwa, mkopo huo utazidisha bajeti ya Sudan Kusini zaidi ya mara dufu.

Msemaji wa serikali mjini Juba, alieleza kuwa fedha hizo zitatumiwa kujenga barabara, daraja na mitandao ya simu, pamoja na kuendeleza kilimo na vinu vya nishati kwenye mito.

Hakutaja mpango wa kujenga bomba la mafuta hadi Bahari ya Hindi.

Uchina inanunua mafuta mengi ya Sudan Kusini, na inataka kubaki na uhusiano mwema na Sudan, mshirika wake wa miaka mingi, na Sudan Kusini, ambayo ilipata uhuru mwaka jana

Mji wa Manchester kuwaka moto

   

Hatumwi mtoto dukani. Ni msemo uliowahi kuusikia mara nyingi, lakini siku ya jumatatu utakua sahihi.

uwanja wa City

Ni siku ambapo wababe wawili wa Ligi kuu ya Premier ya England watapambana ikiwa ni kwenye uwanja wa Etihad wa Manchester City.

Baina ya timu hizi zimefunga bao 173 katika Ligi msimu huu tukishuhudia mengi yaliyofungwa na Wayne Rooney, Sergio Aguero, Javier Hernandez na Carlos Tevez.

Majina haya yanakupa ufahamu kua kila upande unaweza kufanikiwa kuchota pointi kutoka uwanja wa Etihad na kwa ushindi apo Etihad pia Ligi ya msimu huu.

Ukitazama orodha ya majina utaingiwa na tamaa ya ya pambano la kuvutia kutokana na washambuliaji wenye mikwaju mikali bila kusahau wanaowalisha mipira ya kupasua nyavu.

David Silva

Man.City kwa kipindi kirefu imemtegemea David Silva na bado anaweza kushawishi matokeo ya mechi wakati wowote huku United ikimtegemea mno Antonio Valencia aliyekua na ushawishi mkubwa msimu huu kwa kuvunja ngome nyingi za vilabu mbalimbali.

Vijana wa Roberto Mancini walipoteza muelekeo baada ya siku kuu ya Krisimasi kipindi ambapo kiwango cha mcheza kiungo David Silva kilianza kushuka ingawa hivi sasa klabu yake imerejesha uwezo wa kufunga mabao kutokana na hali yake kua bora kwa sasa.

Antonio Valencia

Na huku kurejea kwa mshtuko kwa Paul Scholes mwezi januari kunaweza kuonekana kama changamoto iliyoiwezesha United kupanda kilele cha Ligi kuu, ingawa mchango wa Valencia kutoka upande wa kulia ni mkubwa mno. Valencia.

Kufuatia jeraha la kisiginio la mda mrefu mapema msimu huu Valenzia alizinduka kwa kupachika wavuni bao mbili kati ya 4-1 dhidi ya Wolves tarehe 10 Disemba.

Kwa uchache, hawa ni wawili kati ya orodha ndefu ya wachezaji wa Manchester mbili zinazotambiana kushinda pambano la jumatatu litakaloamua mshindi wa Ligi ya mwaka huu.

Tuangalie uwezekano wa hali inayoweza kujitokeza ikiwa kwa mfano:

City itashinda - basi timu hizi mbili zitakua sawa kwa pointi kukisalia mechi mbili, wingi wa goli za City ukiiweka klabu hio juu ya kilele.

Droo -na hapa United itahitaji pointi nne kutoka mechi zilizobaki, hata ikiwa City itashinda mechi zote zilizobaki.

Hapa ushindi wa United katika mechi itakayofuata dhidi ya Swansea basi itatangazwa United kua mshindi endapo City itashindwa kuifunga Newcastle ugenini.

Endapo United itashinda pambano la jumatatu basi Ligi itahesabu kombe la 20 la United.

Saturday, April 28, 2012

Afisa hataki Israil ishambulie Iran


Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Israil, Shin Bet, amemlaumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, pamoja na Waziri wa Ulinzi, Ehud Barak, kwamba hawawaambii ukweli wananchi wa Israil kuhusu Iran.
Yuval Diskin, mkuu wa zamani wa Shin Bet

Yuval Diskin, amewashutumu wanasiasa hao wawili, kuwa wanafanya uamuzi kwa msingi wa itikadi zao, na alisema hakuna ukweli kwenye hoja yao, kwamba endapo Israil itachukua hatua za kijeshi, Iran haitatengeneza bomu la nuklia.
Juma lilopita mkuu wa jeshi wa Israil aliliambia gazeti moja la nchi hiyo kwamba hafikiri kuwa Iran itatengeneza silaha za nuklia.
Mwezi uliopita, mkuu wa shirika jengine la ujasusi la Israil, Mossad, piya alisema hadharani kuwa anapinga shambulio dhidi ya Iran.

Rais wa Malawi amfuta kazi hasimu wake



Joyce Banda
Rais mpya wa Malawi Joyce Banda amemfuta kazi Waziri wa mambo ya nje Peter Mutharika, kakake Marehemu Rais Bingu Wa Mutharika aliyefariki dunia mwezi huu.
Mutharika alitarajiwa kurithi Marehemu Kakake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2014 ambapo Bingu Wa Mutharika alitarajiwa kustaafu.
Mabadiliko ya baraza la mawaziri yametokea siku chache baada ya maziko ya Rais huyo mapema wiki hii. Bi. Banda amekuwa Makamu wa Rais tangu mwaka 2009 lakini akatofautiana na Wa Mutharika na kuwa mksoaji wake mkubwa.
Kufuatia kifo cha Rais huyo kulizuka wasi wasi kwamba wandani wake wangejaribu kuzuia ukabidhi wa madaraka kwa Bi. Banda ambaye alikuwa na chama chake cha kisiasa.
Miongoni mwa Mawaziri wapya ni Austin Atupele Muluzi, mwanawe Rais wa zamani Bakili Muluzi aliyeteuliwa Waziri wa mipango na ustawi.Wengi waliotimuliwa na waliokuwa wandani wa Bingu Wa Mutharika.

Mauaji ya raia Iraq


Takriban watu thelathini na watano wameuawa katika mfululizo wa mashambulio ya mabomu kote nchini humo.

Katika mji mkuu Baghdad maeneo ya shia, yalilengwa zaidi. Waziri wa Afya Majeed Hamad Amin, amenusurika kuuawa katika eneo hilo wakati bomu lililotegwa garini mwake kulipuka.

Kumekuwa na mashambulio zaidi katika miji ya Kirkuk na Samarra kaskazini mwa nchi hiyo.


Shambulio la bomu Nigeria

 26 Aprili, 2012 

Takriban watu watatu wameuawa katika shambulio lililotokea kwenye ofisi za kampuni moja ya kuchapisha magazeti katika mji mkuu Abuja,Nigeria wafanyakazi wa huduma za dharura wanasema.

Kuna taarifa pia za vifo vya watu wengine watatu baada ya shambulio lingine la bomu katika mji wa kaskazini wa Kaduna kutokea.

Shambulio la mjini Abuja katika kampuni ya gazeti la ThisDay lilitokana na bomu, msemaji wa halmashauri ya shughuli za dharura za kitaifa amesema.

Staruss-Kahn asema alitoswa na Sarkozy

 28 Aprili, 2012 

Dominique Strauss-Kahn, mkuu wa zamani wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, anasema anaamini kashfa iliyomuandama baada ya kashfa iliyohusu mapenz , ilichochewa na watu waliohusika na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.

Dominique Staruss-Kahn

Bwana Strauss-Kahn alijiuzulu baada ya kutuhumiwa kumbaka mfanyakazi wa hoteli mjini New York.

Hakusema kama alitegwa kukumbana na msichana huyo, lakini anadai kuwa matukio yaliyofuata yalikuwa njama ili kuhakikisha kuwa anaaibika hadharani.

Kabla ya kashfa hiyo, Bwana Strauss-Kahn akitarajiwa kumpinga Bwana Sarkozy kuania urais.

Mwandishi wa BBC anasema mahojiano hayo yametoka wakati tete, juma moja tu kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.


BAADHI YA MARAIS WA (EAC) WAWASILI JIJINI ARUSHA

Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya akipokelewa na Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika mjini Arusha tarehe 28 Aprili, 2012.

Mhe. Rais Kibaki akifurahia burudani ya ngoma mara baada ya kuwasili KIA.

Mhe. Rais Kibaki akiwa na wenyeji wake Mhe. Membe (kulia) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta (kushoto) mara baada ya kuwasili KIA

Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Uganda akisalimiana na Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 28 Aprili, 2012.

KITIVO CHA ELIMU UDOM CHAIBUKA NA USHINDI WA VIKAPU 58 KWA 53 DHIDI YA DODOMA SPURS KATIKA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU MKOANI DODOMA

Mchezaji wa timu ya Kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma akijaribu kufunga katika mechi ya ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo na timu hiyo ya walimu kuibuka washindi kwa vikapu 58 kwa 53 dhidi ya Timu ya Kikapu Ya Mkoa Wa Dodoma

Mpira ukiingia kwenye nyavu na kupelekea timu ya kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma kushinda

Mchezaji wa timu ya Kitivo cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma akiokoa hatari goli kwake

Kashikashi ikiendelea hapo huku wengine wakitaka kushinda huku wengine wakitaka kuokoa goli lisiingie

Mchezaji wa Timu ya Mkoa alipoipatia timu goli katika ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo katika viwanja vya kitivo cha sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha cha Chuo Kikuu Cha Dodoma

Mchezaji wa Timu ya Kikapu ya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) akijaribu kumpita Mchezaji wa timu ya kikapu ya kitivo cha elimu cha chuo kikuu cha Dodoma katika mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo na timu ya Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Chaibuka Mshindi Kwa Vikapu 58 kwa 53 Dhidi ya Timu ya Mkoa (DODOMA SPURS)

 Mpira ukielekea nyavuni hapo

Benchi la Makamisaa likifuatilia Mchezo huo Kwa Makini

 Baadhi ya Wanafunzi na Wadau wengine wakifuatilia mchezo huo uliokuwa ukichezwa kati ya Timu ya Mpira ya Kikapu kutoka Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Timu ya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) ambapo timu ya kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma iliibuka na ushindi wa Vikapu 58 kwa 53 dhidi ya Timu ya Mkoa Wa Dodoma (DODOMA SPURS) katika ligi ya mpira wa kikapu inayoendelea kufanyika katika viwanja vya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii,Sanaa na Lugha cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)

Friday, April 27, 2012


Pep Guardiola kuondoka Barcelona

 
Pep
Josep Guardiola kutangaza kuondoka Bacra
Inafahamika kuwa Pep Guardiola anakaribia kuacha kuifundisha Barcelona baada ya kuifahamisha klabu hiyo kuwa hawezi kuendelea kuwa kocha.
Guardiola mwenye umri wa miaka 41 atatangaza nia yake hiyo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa alasiri.
Iwapo hatobadili mawazo yake, Guardiola anatarajiwa kuthibitisha habari za kuondoka katika timu aliyoipa ushindi wa Klabu Bingwa Ulaya mara mbili. Meneja huyo amepanga kukutana na wachezaji asubuhi ya Ijumaa.
Inadhaniwa kuwa Guardiola atachukua mapumziko ya mwaka mmoja kufundisha soka, iwapo atatangaza uamuzi wa kuacha nafasi yake hiyo.
Guardiola alikutana na rais wa Barcelona Sandro Rossell kwa muda wa saa tatu siku ya Alhamisi asubuhi.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Rossell mjini Barcelona, Guardiola anasemekana alionesha kuwa "hawezi kuendelea tena".
Mazungumzo yaliyoanza kuhusu kuongeza mkataba wake wa kila mwaka, kwa mwaka mmoja, yalibadilika na kuwa ya kumshawishi asiondoke kabisa. Inafahamika kuwa Rossell amempa Guardiola uwezo wa kutumia kiwango anachotaka kusajili, lakini kocha huyo hakuchukua uamuzi wake kuhusiana na fedha.
Guardiola ambaye alikuwa nahodha wa Barcelona wakati akicheza soka, amekuwa akisisitiza kuwa atafanya kila awezalo kusaidia klabu hiyo. Alitumia siku ya alhamisi mchana akiwa na familia yake na anatarajiwa kumwambia Rossell uamizi wake baadaye usiku.
Wakati uwezekano wake wa kubadili mawazo bado upo, klabu hiyo ina wasiwasi kuwa mtu aliyewaongoza kunyakua makombe mawili ya Klabu Bingwa Ulaya na vikombe vitatu vya ligi kuu huenda amekwisha fanya uamuzi wake.
Jinsi Barca walivyofungwa na Real Madrid siku ya Jumamosi, matokeo ambayo yalididimiza matumaini ya kuchukua uningwa wa ligi kuu na pia kutolewa na Chelsea katika Klabu Bingwa Ulaya ndio kumesababisha uamuzi wake huo.

TUNDU LISSU ASHINDA KESI YA KUPINGA UBUNGE WAKE

 
  • Hoja zote za upande wa mlalamikaji zatupwa.
  • Maofisa Jeshi pamoja na kikosi maalum waudhulia maakamani.
Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, ameshinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake mjini Singida kupinga ushindi uliomweka madarakani
Hukumu imetolewa na Jaji Moses Mzuna anayetoka mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.
 
Leo mahakamani wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari walijitokeza kwa wingi sana katika eneo la mahakama.

Idadi ya Polisi pia ilikuwa kubwa, ndani na nje ya mahakama.Kilicho kuwa cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa jeshi la polisi walikuwepo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kukagua kila anayeingia mahakamani,  kila mtu aliyekuwa anaingia mahakamani alipekuliwa hadi wabunge waliokuja kusikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu Jaji Moses Mzuna alisema “HOJA YA TISA, Kama Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo. Hoja hii haipaswi kunipotezea muda sana. Njau hakuhudhuria, aliwakilishwa na mlalamikaji wa kwanza ambaye alikataa kusaini matokeo.

Wakili wa serikali alisema, kukataa pekee kusaini matokeo hakusaidii kutengua matokeo. Hivyo hata hoja ya tisa naitupilia mbali. Haikuwa sahihi.
Hoja ilitolewa hapa, kuwa mawakala walikula kiapo kwa hakimu. Walalamikaji walisema kuwa walipaswa kula kiapo kwa msimamizi wa uchaguzi. Je kuapishwa na hakimu kunabatilisha matokeo?

Hoja zilizotolewa na mawakili wa serikali walisema Hakimu ana mamlaka ya kutoa viapo. Binafsi nasema kuwa waliotunga sheria hawakumaanisha kuwa Mahakimu hawaruhusiwi kuapisha mawakala, vinginevyo kungekuwepo fomu ya hakimu tu. Lakini fomu zinaonyesha hakimu, Msimamizi wa uchaguzi na Msimamizi msaidizi, fomu inatambulika kisheria, kwa sheria ya Uchaguzi. Hii haihusiani na zoezi la uchaguzi.

Katika kesi ya Prince bagenda Vs Wilson masilingi, katika kesi hii mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240.

Kwa lugha yake jaji alisema hawakuwa na mamlaka halali, lawful mandate, lakini ilisaidia kutengua, na mwanasheria wa serikali alihusika katika hili.

Maelezo hayo yanatofautiana na kesi iliyo mbele yangu, jimbo la Singida mashariki mawakala walikula kiapo, na walikuwa na mamlaka halali. Hivyo hoja hii naitupilia mbali

HIVYO, UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI, NA TUNDU LISSU NI MBUNGE HALALI NA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA WA HAKI, HIVYO SIWEZI KUTENGUA.

Walalamikaji wa kesi hiyo, iliyofunguliwa mahakama kuu kanda ya Dodoma, walikuwa wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kutoka mkoani Dodoma, huku Lissu akijisimamia mwenyewe.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa CCM, kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na dosari nyingi.

Awali Katika mahojiano na Lissu, alisema vyovyote mahakama itakavyo hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa mbunge wa kwanza kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati.

Waandamana nusu uchi kulalamikia polisi

wanawake Uganda
Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.
Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.
Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.

Katibu Mkuu wa UN akemea hatua ya Sudan

Soko moja lilinyeshewa kwa mabomu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini.
Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.
Awali, Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE kujulikana mei 5 NDANI YA HOTELi YA KITALII YA NAURA SPRINGS


Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/= 

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo

Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S  ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.

Katibu Mkuu wa UN akemea hatua ya Sudan

Soko moja lilinyeshewa kwa mabomu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini.
Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.
Awali, Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE kujulikana mei 5 NDANI YA HOTELi YA KITALII YA NAURA SPRINGS


Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/= 

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo

Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S  ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.