Staruss-Kahn asema alitoswa na Sarkozy
Dominique Strauss-Kahn, mkuu wa
zamani wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, anasema anaamini kashfa
iliyomuandama baada ya kashfa iliyohusu mapenz , ilichochewa na watu
waliohusika na rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.
Bwana Strauss-Kahn alijiuzulu baada ya kutuhumiwa kumbaka mfanyakazi wa hoteli mjini New York.
Hakusema kama alitegwa kukumbana na msichana
huyo, lakini anadai kuwa matukio yaliyofuata yalikuwa njama ili
kuhakikisha kuwa anaaibika hadharani.
Kabla ya kashfa hiyo, Bwana Strauss-Kahn akitarajiwa kumpinga Bwana Sarkozy kuania urais.
Mwandishi wa BBC anasema mahojiano hayo yametoka wakati tete, juma moja tu kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.
No comments:
Post a Comment