Sunday, April 29, 2012
Mripuko kwenye kanisa mjini Nairobi, Kenya, umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine 10.
Polisi wanasema guruneti lilirushwa kwenye kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, wakati wa ibada ya asubuhi.
Daktari mmoja katika Guru Nanak Hospital mjini Nairobi, ambako ndiko majeruhi walikopelekwa, aliwaelezea waandishi wa habari majeruhi aliowaona:
"Tumepokea majeruhi 7, mwanamke mmoja aliumia vibaya kwenye mguu wa kushoto, ambao umevunjika mahala kadha.
Mwanamme mmoja alikuwa na majaraha kadha kwenye nyama na tunafikiri amevunja mifupa piya; labda tukimfanyia x-ray tutatambua.
Kuna mama mmoja aliyevunja kidogo kisuguru cha mguu wa kushoto, na wengineo wamepata mikwaruzo-kwaruzo na kujikata-kata."
Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment