Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya akipokelewa na Mhe. Bernard K.
Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara
alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
jana kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki utakaofanyika mjini Arusha tarehe 28 Aprili, 2012.
Mhe. Rais Kibaki akifurahia burudani ya ngoma mara baada ya kuwasili KIA.
Mhe. Rais Kibaki akiwa na wenyeji wake Mhe. Membe (kulia) na
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samwel Sitta (kushoto)
mara baada ya kuwasili KIA
Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Uganda akisalimiana na Mhe. Samwel
Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili
KIA kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki tarehe 28 Aprili, 2012.
Mchezaji wa timu ya Kitivo cha elimu
cha Chuo Kikuu Cha Dodoma akijaribu kufunga katika mechi ya ligi ya
mpira wa kikapu iliyoanza leo na timu hiyo ya walimu kuibuka washindi
kwa vikapu 58 kwa 53 dhidi ya Timu ya Kikapu Ya Mkoa Wa Dodoma
Mpira ukiingia kwenye nyavu na kupelekea timu ya kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma kushinda
Mchezaji wa timu ya Kitivo cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma akiokoa hatari goli kwake
Kashikashi ikiendelea hapo huku wengine wakitaka kushinda huku wengine wakitaka kuokoa goli lisiingie
Mchezaji wa Timu ya Mkoa alipoipatia
timu goli katika ligi ya mpira wa kikapu iliyoanza leo katika viwanja
vya kitivo cha sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha cha Chuo Kikuu Cha
Dodoma
Mchezaji wa Timu ya Kikapu ya Dodoma
Spurs (Timu ya Mkoa) akijaribu kumpita Mchezaji wa timu ya kikapu ya
kitivo cha elimu cha chuo kikuu cha Dodoma katika mchezo wa ligi ya
mpira wa kikapu iliyoanza leo na timu ya Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu
Cha Dodoma Chaibuka Mshindi Kwa Vikapu 58 kwa 53 Dhidi ya Timu ya Mkoa
(DODOMA SPURS)
Mpira ukielekea nyavuni hapo
Benchi la Makamisaa likifuatilia Mchezo huo Kwa Makini
Baadhi
ya Wanafunzi na Wadau wengine wakifuatilia mchezo huo uliokuwa
ukichezwa kati ya Timu ya Mpira ya Kikapu kutoka Kitivo Cha Elimu Cha
Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Timu ya Dodoma Spurs (Timu ya Mkoa) ambapo timu
ya kitivo cha elimu cha Chuo Kikuu Cha Dodoma iliibuka na ushindi wa
Vikapu 58 kwa 53 dhidi ya Timu ya Mkoa Wa Dodoma (DODOMA SPURS) katika
ligi ya mpira wa kikapu inayoendelea kufanyika katika viwanja vya Kitivo
Cha Sayansi ya Jamii,Sanaa na Lugha cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
No comments:
Post a Comment