Wigan imeendelea kuonesha kandanda maridadi baada ya kuillaza Newcastle mabao 4-0 na kudhihirisha nia ya kujinusuru kuteremka daraja, matokeo ambayo pia yameivurugia Newcastle nafasi ya kuikalia nafasi ya tatu hatimaye kucheza moja kwa moja Ligi ya Ulaya msimu ujao.
Shaun Maloney akaongeza bao la tatu na kujihakikishia ushindi kabla ya Franco di Santo kushindilia msumari wa mwisho kabla ya mapumziko na ubao wa mabao ukasomeka Wigan 4 Newcastle 0.
Papiss Cisse ambaye tangu ajiunge na Newcastle amekuwa akipachika mabao karibu kila mchezo, mkwaju wake uligonga mwamba lakini hata hivyo timu hiyo ilionekana wanyonge kwa Wigan na kuziachia pointi tatu muhimu.
Huu ni ushindi wa tano wa Wigan katika mechi sita zilizopita na kusogea pointi tatu mbele kutoka eneo la hatari la kuteremka daraja wakisaliwa na mechi mbili kabla hawajamaliza msimu.
Arsenal ilisogea karibu kuishika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kulazimishwa sare na Stoke.
The Gunners walianza kufungwa baada ya Peter Crouch kuunganisha kwa kichwa mpira wa juu uliopigwa pembeni na Matthew Etherington.
Arsenal haraka wakajibu shambulio wakati Tomas Rosicky pasi yake ya pembeni ilipounganishwa wavuni na Robin van Persie.
Yossi Benayoun alinyimwa mkwaju wa penalti baada ya Glenn Whelan kumuangusha ndani ya eneo la hatari wakati muda ukiwa umeyoyoma na timu zote zikiwa zimeridhika kwa kugawana pointi moja moja.
Nikica Jelavic aliifungia Everton mabao mawili ikiwa ni hatua moja mbele juu ya Liverpool wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa kupendeza wa mabao 4-0 dhidi ya Fulham katika uwanja wa Goodison Park.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Croatia alifunga mabao yake hayo mawili katika kipindi cha kwanza na kabla ya mapumziko Marouane Fellaini aliongeza bao la tatu.
Tim Cahill aliyeingia kipindi cha pili aliiongezea Everton bao la nne, wakati Fulham wakiwa wamekwisha sambaratika.
Ushindi huo umeinyanyua Everton hadi nafasi ya saba, wakiwa pointi tano zaidi ya Fulham.
Everton wanamaliza msimu kwa kishindo huku meneja wao David Moyes akiwa na nia ya kukamata nafasi nane bora za juu baada ya muda wa miaka 11.
Everton haijawahi kumaliza juu ya Liverpool katika msimamo wa Ligi Kuu ya England tangu mwaka 2005, lakini huu ni msimu wao wa tatu wenye manufaa.
Kevin Davies alifunga mabao mawili na kuipatia pointi moja Bolton wakati Sunderland iliposhindwa kuendeleza wimbi la ushindi kwa mchezo wa tano.
Nahodha huyo wa Bolton alijaza mpira wa juu wavuni kufuatia pasi ya pembeni ya Martin Petrov kabla Nicklas Bendtner kuisawazishia Sunderland.
Mkwaju wa James McClean wa adhabu ya moja kwa moja uliipatia Sunderland bao la pili kabla Davies tena hajaiokoa Bolton kwa kusawazisha na kuionesha Sunderland kwa nini walitaka kumsajili mwezi wa Januari.
Nayo Aston Villa iliambulia pointi moja baada ya kuilazimisha West Brom kutoka sare ya kutofungana.
Villa walipata nafasi nzuri kipindi cha kwanza, wakati Gabriel Agbonlahor mara mbili mikwaju yake ilipookolewa na mlinda mlango wa West Brom Ben Foster.
Lakini wenyeji walinyimwa mkwaju wa penalti baada ya mapumziko wakati Alan Hutton alipozuia mpira wa kichwa uliopigwa na Liam Ridgewell na kumgonga mkononi na kupaa juu ya lango.
Timu zote mbili zilipata nafasi nzuri wakati mpira ukielekea kumalizika.
Mabao mawili ya Matt Jarvis yaliiwezesha Wolves kupigana kiume na kuilazimisha Swansea kutoka nayo sare ya mabao 4-4 katika pambano zuri na la kusisimua.
Pambano hilo lililoanza kwa kasi tangu mwanzo lilishuhudia Andrea Orlandi na Nathan Dyer wakipachika mabao ya haraka haraka Swansea.
Steven Fletcher wa Wolves aliuchepua kwa kichwa na kufunga bao la kwanza akijibu shambulio la Swansea kabla ya mpira wa pembeni wa Danny Graham kujaa wavuni na ubao wa mabao ukasomeka 4-1. Baadae Jarvis akafanikiwa kuweka wavuni mabao mawili na kuikoa Wolves kwa kipigo kingine.
Wolves waliingia uwanja wa Liberty Stadium wakiwa mkiani mwa msimamo wa ligi na tayari wameshateremka daraja na dalili za awali zilionesha watashindiliwa kucheza ligi ya Championship kwa kuvurumishiwa mabao mengi hali ambayo ikawa tofauti
No comments:
Post a Comment