Friday, May 4, 2012

Chelsea kununua kituo cha Battersea

Kituo cha Battersea
Chelsea ina mipango ya kutobomoa mabomba ya kutolea moshi ikiwa itajenga uwanja mpya katika kituo cha Battersea
Chelsea imewasilisha ombi la kutaka kukinunua kituo cha kuzalisha umeme cha Battersea mjini London, na klabu kina mipango ya kujenga uwanja mpya wa soka mahali hapo, utakaoweza kuwapokea mashabiki 60,000.
Mabomba manne ya kutolea moshi katika uwanja huo yatabaki, na kuwa ni sehemu moja ya upande wa kusini mwa uwanja itakayokuwa na viti 15,000.
Chelsea imeelezea imekuwa vigumu kupanua uwanja wao wa Stamford Bridge, na kiuchumi, mpango huo haufai, na vile vile klabu kimekuwa na matatizo katika kuwashawishi wahusika kuidhinisha mipango yake ya upanuzi.
Klabu kimeongezea kwamba kuna wengine wanaotaka kukinunua kituo hicho.
"Hakuna uhakika kwamba ombi letu litafaulu," taarifa ya klabu imeelezea.
"Lazima pia kusisitiza kwamba kwa kuwasilisha ombi la kukitaka kituo cha Battersea cha kuzalisha umeme, hayo hayamaanishi moja kwa moja uamuzi kamili wa kuuhama uwanja wa Stamford Bridge."
Klabu kimeelezea kwamba kitazingatia masharti ya kutobomoa ukumbi uliopo katika eneo hilo na pia chumba cha kuendesha mitambo ya umeme, kwa kuzingatia sheria zinazohusiana na kuhifadhi majumba ya kale.
Kufanya hivyo itakuwa ni nafasi ya kujenga uwanja wa kupendeza wa kisasa, lakini pia kwa kuhifadhi na kuimarisha mandhari ya eneo hilo.
Klabu pia kina mipango ya kujenga maduka, nyumba na afisi katika eneo hilo, na vile vile kuimarisha usafiri kupitia treni za chini kwa chini
Uwanja wa Stamford Bridge, unaoweza kuruhusu mashabiki 42,000, hauwezi kulinganishwa na uwanja wa kisasa kabisa wa Imarati wa Arsenal, ambao unaweza kuingiza mashabiki 60,000, huku ule wa Manchester United wa Old Trafford ukiwa na uwezo wa kuwaruhusu mashabiki 76,000.

No comments:

Post a Comment