Friday, May 4, 2012

MAHARAMIA WA CHAFUA HALI YA HEWA KIGOMA


Askari wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kwa kushirikiana na askari wa jeshi la polisi mkoani Kigoma wamepambana kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni maharamia waliokuwa wamevamia wavuvi na kupora injini za boti katika ziwa Tanganyika
Taarifa za kipolisi zimesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kudumu kwa kutwa nzima ya leo ambapo askari watatu wa JWTZ na wawili wa jeshi la polisi akiwemo OC CID Mohamed Kilonzo wamejeruhiwa vibaya na wamelazwa kwene chumba cha upasuaji katika hospitali ya mkoa ya Maweni
Mkuu wa wilaya ya Kigoma John Mongella amewaambia waandishi wa habari kuwa ulitokea uharamia ziwani na wananchi wakasaidia katika kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama na ndipo vyombo vya vikaenda kusaidia lakini akasema ni mapema sana kusema mengi kuhusiana na tukio hilo

No comments:

Post a Comment