Thursday, June 21, 2012

JACK DUSTAN AWEKWA KINYUMBA HOTELINI


 Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’.
Na Gladness Mallya
MSHIRIKI wa Shindano la Maisha Plus Season II, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’ anadaiwa kuwekwa kinyumba hotelini kwa muda wa wiki moja.
Kikizungumza chanzo makini ambacho ni rafiki wa karibu na Jack kilisema kuwa mwanadada huyo aliwekwa katika Hoteli ya Danfrense iliyopo maeneo ya Sinza White Inn, Dar ambapo alikaa na mwanaume mmoja ambaye hakujulikana jina anayeishi nchini Denmark.
“Yaani Jack alikaa hotelini kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya huyo mwanaume wake, naona huyo ndiyo anampa mkwanja ‘so’ yupo tayari kwa lolote,” kilisema chanzo.
Jack alipopatikana alifunguka: “Ni kweli nimekaa hotelini na mwanaume wangu anayeishi Denmark, siwezi kumtaja, alikuja kwa ajili yangu. Pia siwezi kusema ni mchumba wangu kwa sababu bado hajajitambulisha kwetu lakini naweza kusema ni mpenzi wangu tu na ameshaondoka.”

No comments:

Post a Comment