Tuesday, June 19, 2012

MSANII WA FILAMU APIGA PICHA CHAFU


Esha Salim Buheti.
Na Musa Mateja
STAA wa filamu ambaye havumi lakini yumo, Esha Salim Buheti aliyecheza filamu za Mrembo Kikojozi, Kinyonga, Kisasi cha Utata na nyinginezo amejikuta akitengeneza kichwa cha habari kwa mara ya kwanza baada ya picha zake chafu kunaswa.
Picha hizo zinamuonesha demu huyo akiwa ameacha wazi sehemu nyeti za mwili wake ambazo kwa maadili ya Kibongo anayestahili kuziona ni ‘mtu’ wake tu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichoomba hifadhi ya jina lake, picha hizo alikuwa akimtumia mshikaji wake aishie nchi za nje lakini kwa bahati mbaya zikivuja na kutua kwenye dawati letu.
Akizungumza na Ijumaa, msanii huyo alisema picha anazozijua ni zile alizopiga akiwa klabu na marafiki zake na akadai eti wakati anazipiga alikuwa amekaa vibaya hivyo maeneo yake muhimu kuonekana.
“Jamani mimi siyo mtu wa skendo, hata ndugu zangu wananijua na hizo picha nilipiga klabu jamani na si kwa nia mbaya lakini kama kuna nyingine hizo sizijui,” alisema msanii huyo.

No comments:

Post a Comment