aturday, June 16, 2012
Na Grace Soka, Afisa Uhusiano wa Mt. Kilimanjaro Marathon.
Mcheza sinema maarufu duniani kutoka
nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount
Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni
mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.
Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie
France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka
1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi
kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.
Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza
sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great
Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na
kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz
alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika
jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini
Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira
Films LLS.
eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya
mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana
kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani
wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea
kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika
bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka
jana.
Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie
Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani.
Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja
na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja
kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa
wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya
mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.
Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi
Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta
42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa
watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote
wanaweza kukimbia.
No comments:
Post a Comment