Sunday, June 3, 2012
Bendi dansi ya FM maarufu kama wazee
WANGWASUMA pamoja na msanii wa vichekesho MPOKI watatoa burudani ya
anina yake katika shindano la kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni
City 2012' litakalofanyika Juni 15 mwaka huu katika ukumbi wa Navy
Beach ulioko huko Kigamboni hapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa
shindano hilo, Somoe Ng'itu, bendi ya FM inafahamika kwa kutoa burudani
nzuri kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini.
Kuhusiana na msanii MPOKI, SOMOE amesema
kuwa mchekeshaji huyo ambaye pia ni mkazi wa KIGAMBONI amekuwa ni kati
ya waburudishaji katika sanaa ya uchekeshaji na kupendwa na watu wa rika
zote hivyo mashabiki wa urembo wataweza kupata burudani ya uhakika.
Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L,
alisema kuwa Jumla ya warembo 15 wanaendelea kujifua katika kambi ya
mazoezi chini ya mwalimu wao miss TEMEKE HAWA ISMAIL ambaye
anashirikiana na mshiriki wa miss TANZANIA mwaka jana BLESSING NGOWI.
Amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na
CAROLYNE DANDU, FATINA FRANSIS, EDDA SLYVESTER, AISHA MUSSA, ROSEMARY
PETER, DOREEN KWEKA,CAROLINE PETER, AGNES GOODLUCK, SOPHIA MARTINE,
ROSEMARY DEOGRATIUS, BEATRICE BONIFACE, JULIETH PHILIP na KHADIJA KOMBO.
"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji,
tunaamini shindano letu litakuwa na mvuto na hadhi ya kipekee kama eneo
lake lilivyo," aliongeza.
Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri
watapata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika mashindano ya
kanda ambayo yatafanyika baadaye mwaka huu.
Aliwataja wadhamini ambao tayari
wamethibitisha kudhamini shindano hilo ni pamoja na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine na NSSF,
Hope country Motel, Norbro’s Collections, Screen masters, Global
Publishers.
Salha Israel kutoka Kanda ya Ilala ndiye
mrembo anayeshikilia taji la taifa ambapo mwaka huu ratiba ya mashindano
hayo imebadilika.
No comments:
Post a Comment