Friday, May 11, 2012
AGNESS MASOGANGE AWACHAMBA MASTAA WA MOVIE
MWANANADADA tishio katika kupamba video za wanamuziki mbalimbali nchini Agnes Gerald maarufu kama Agnes Masogange ameweka wazi kuchukizwa na tabia ya mastaa wa kike wa bongo muvie kuwadharau wasichana 'wanaouza sura' (video Queen). Mwanadada huyo mwenye umbo la utata, ambaye kuzitendea haki fedha anazolipwa kwa 'kuuza sura' alisema kwamba tabia hiyo iliyokithiri imekuwa ikonekana mara nyingi wanapokutana katika mikusanyiko mbalimbali ikiwemo kwenye kumbi za starehe ambapo mastaa wa bongo movie huwaona video Queen hao kuwa si lolote. "nawashangaa sana na hizi tabia zao kwani kazi ni kazi tu kama ilivyokwao katika kuigiza, kikubwa ni kila mtu anakula kwa jasho lake...nashangaa wanavyotunyanyapaa tunapokutana klabu,"alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment