Wednesday, May 30, 2012

WEMA SEPETU ARUSHA ROHO YA JOKATE



Msanii ambaye hajawahi kukaukiwa na matukio yenye kufaa kutengeneza vichwa vya habari katika vyombo vya habari nchini, Wema Abraham Sepetu, kwa mara nyingine ametawala vyombo vya habari baada ya tukio lake la usiku wa jana la kuvishwa pete ya uchumba na msanii wa bendi ya Machozi, anayekwenda kwa jina la Mwinyi.
Tukio hilo ambalo limevuta hisia za wapenzi wa masuala ya udaku na burudani nchini, lilijiri katika ukumbi wa Maisha Club, jijini dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, ambapo lilishuhudiwa na mashabiki lukuki wa bendi ya Machozi waliokuwa wamejazana hapo kwa ajili ya burudani ya muziki uliokuwa ukiporomoshwa na bendi hiyo.
Hata hivyo, tofauti na ambavyo imechukuliwa na watu wengi kuwa Wema amepata mchumba mpya na ndio alikuwa akimvisha rasmi pete ya uchumba, ukweli ambao umewekwa wazi ni kuwa, mwanadada huyo alihusika katika tukio hilo kama sehemu ya maandalizi ya filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la Super Star.
Movie hiyo inatarajiwa kuelezea maisha halisi ya msanii huyo ambaye pia aliwika katika medani za ulimbwende, na Mwinyi atashiriki katika filamu hiyo akiigiza nafasi ya mwanamuziki Diamond, ambaye alikuwa mpenzi wa Wema na ambaye alimvisha pete ya uchumba lakini wakamwagana baadae kutokana na mikasa baina yao kuzidi kushamiri.
Kibwagizo: Hata hivyo, Wema anajulikana kuwa hajatulia, unadhani itashangaza kesho kusikia kuwa tukio hilo mbali ya kuwa sehemu ya filamu, lilikuwa pia tukio rasmi la kuwaunganisha wawili hao?

No comments:

Post a Comment