Nchini Italia Alessandro del Piero alifunga bao lake la mwisho ikiwa ndiyo mara ya mwisho kuiwakilisha klabu ya Juventus kama bingwa mpya wa Ligi ya Sere A baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Atalanta jumapili.
Inzaghi alifunga bao kuisaidi Milan katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Novara. Hata hivyo ushindi huo haukuwa na maana yoyote kwa sababu Juventus tayari ilikua inaongoza kwa pointi 4 kabla ya mechi ya mwisho na kujishindia Ligi ya msimu ikiwa ni ushindi wa mara 28.
Mji wa Turin ulikua katika hali ya sherehe ambapo maelfu ya mashabiki walimiminika mitaani kushereheka ushindi wa kwanza baada ya miaka 9.
Mjini Geneva matokeo ya jumapili FC Zürich 0 Servette 1, Thun 2 Young Boys 2, na jumamosi Basel 6 Grasshoppers 3, Lucerne 3 Lausanne-Sport 2.
Kwa matokeo hayo Salzburg ilijishindia Ligi ya Austria kwa mara ya 7 kwa mabao 5-1 katika mechi yao ya mwisho kwenye uwanja wa Wiener Neustadt.
No comments:
Post a Comment