Askari wa
jeshi la wananchi Tanzania JWTZ kwa kushirikiana na askari wa jeshi la polisi
mkoani Kigoma wamepambana kwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni maharamia
waliokuwa wamevamia wavuvi na kupora injini za boti katika ziwa Tanganyika
Taarifa za
kipolisi zimesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kudumu kwa
kutwa nzima ya leo ambapo askari watatu wa JWTZ na wawili wa jeshi la polisi
akiwemo OC CID Mohamed Kilonzo wamejeruhiwa vibaya na wamelazwa kwene chumba
cha upasuaji katika hospitali ya mkoa ya Maweni
Mkuu wa
wilaya ya Kigoma John Mongella amewaambia waandishi wa habari kuwa ulitokea
uharamia ziwani na wananchi wakasaidia katika kutoa taarifa kwa vyombo vya
usalama na ndipo vyombo vya vikaenda kusaidia lakini akasema ni mapema sana
kusema mengi kuhusiana na tukio hilo
No comments:
Post a Comment