Monday, May 21, 2012

Msafara wa Chelsea London magharibi


Maelfu kwa maelfu ya mashabiki wanaimba na kushangilia kikosi cha Chelsea kilichoshinda Ligi ya mabingwa baada ya kurejea kutoka Munich kupitia mitaa ya London ya magharibi.
Timu ya Chelsea ikisafiri juu ya mabasi mawili yaliyo wazi, ilianza msafara wake kutoka uwanja wa Stamford Bridge majira ya adhuhuri hapa London.
Chelsea au maarufu kama The Blues' ilifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya mabingwa kwa kuibwaga klabu iliyo shinda kombe le mshindi mara nne, Bayern Munich huko Ujerumani.
Ushindi wa kwanza
Ushindi wa kwanza
Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya London kushinda kombe la Ulaya.
Basi ambalo Timu ya Chelsea ilisafiria, limepambwa kwa rangi za klabu, na limekua likisimama kwenye kila hatua ambapo wachezaji wakiliinua Kombe kuwaonyesha mashabiki waengi ambao wamekua wakijitokeza kwa masaa mengi.
Mashabiki wamekua wakiwarushia wachezaji mawele kama ishara ya kuwaenzi -desturi iliyoanza mwishoni mwa miaka ya 1980, mashabiki walipoanzisha tabia ya kurusha figili angani, na kufuatiwa na nyimbo.
Stamford bridge
Stamford bridge
Baadaye klabu ya Chelsea ikapiga marufuku figili kutumiwa ndani ya uwanja wa Stamford Bridge.
Mwandishi wa BBC aliyeshuhudia sherehe hizo Ed Davey, amesema kua mashabiki walirusha vijiti vya figili wakati wakisubiri msafara, lakini walikua wachangamfu waliojaa nidhamu.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema si jambo la kawaida kuiona timu kutoka Uingereza ikishindana kupiga mashuti ya matuta dhidi ya klabu kutoka Ujerumani na Waingereza kushinda.
Nilishuhudia yote hayo nikiwa pamoja na Chancellor wa Ujerumani, ulikuwa wakati mgumu kusubiri kuona mshindi, lakini baadaye tulipongezana,alisema Waziri Mkuu.

No comments:

Post a Comment