Monday, May 28, 2012

DIAMOND ALIPOFUNIKA BIG BROTHER STARGAME

  MWANAMUZIKI nyota wa Tanzania wa Bongo flava, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz” juzi usiku aliweza kuuteka umati wa wageni maalum uliofurika kwenye ukumbi wa  jumba la shindano la Big Brothe stargame, na afrika kwa ujumla kwa kupiga shoo kali na ya aina yake ,nchini Afrika Kusini.
Katika shoo hiyo ambayo pia ilishuhudiwa na mamilioni ya watazamaji, ulimwenguni kote kupitia ving’amuzi vya Dstv,  Diamond aliweza kudhihirisha uwezo wake huo kwa kuangusha bonge la shoo  ikiwemo kwa wimbo wake wa ‘Mawazo’ ambao  uliwachanganya watu mbalimbali na kuamka vitini mwao na kupanda  jukwaani na kucheza nae.
Diamond kama kawaida yake, aliweza kuvalia vilivyo, alikonga nyoyo za mashabiki hao kwa staili yake ya uchezaji ikiwemo ya kuigiza kama anaanguka pamoja na ile ya miondoko ya msanii wa Orijino komed, Joti, hadi anamaliza shoo hiyo mashabiki hao walikua na hamu ya kumuona na kusikia nyimbo zake.
Awamu ya pili, Mshereheshaji mkuu wa shindano hilo, Osakioduwa maalufu, IK, aliweza kumwita tena jukwaani Diamond ilikuzungumza machache, Diamond bila hiyana aliwashukuru mashabiki kwa sapoti waliompa na kuwapongeza wote.

“Nimefarijika sana,nawapendeni wote Big brother, funs, na wote” alisema Diamond na baadae IK, alimuomba apige wimbo wa mwisho wa kufungia shoo hiyo na kuporomosha kibao cha ‘Moyo wangu’ ambacho nacho kiliwachanganya zaidi mashabiki huku kivutio lkikubwa kikiwa juu ya uchezaji wake huo wa Kijoti.
Katika shoo, hiyo, mshiriki wa Zambia, Mampi aliweza kutolewa kufuatia kupata kura chache zilizopigwa baada ya kuingia kwenye hatari yeye na wenzake wawili,Maneta na Lady May.

No comments:

Post a Comment