Mapigano makali yamezuka
mwashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wakati muda uliotolewa
kwa wanajeshi walioasi kujisalimisha.
Maelfu ya wanavijiji walikimbia kuvuka mpaka na kuingia Uganda usiku, maafisa wa Uganda waliiambia BBC.Mwishoni mwa wiki iliyopita jeshi liliwapa mamia ya wanajeshi walioasi mwezi uliopita siku tano wajisalimishe wenyewe.
Wanamtii Bosco Ntaganda, anayejulikana kama"Terminator" na anatakiwa na ICC kwa tuhuma za uhalifu wa kivita.
Mahakama ya ICC inamtuhumu Jenerali Ntaganda kwa kuwasajili watoto kuwa askari kwa kundi hilo hilo la waasi kama ilivyokuwa kwa Thomas Lubanga, ambaye mwezi Machi alikuwa mtu wa kwanza kukutwa na hatia na Mahakama hiyo.
Jenerali huyo aliyepigana katika makundi mbalimbali ya wapiganaji kwa miaka mingi anakataa kupanga uasi na wapiganaji wa kundi la CNDP
Hawa wapiganaji wa CNDP walijiunga na jeshi la Kongo kama sehemu ya mpango wa amani miaka mitatu iliyopita.
'Kujiunga upya'
Watu wa Kongo ambao wanawasili Uganda kwa maelfu wanasema wanakimbia kwa sababu ya kusikia majibizano makali ya risasi karibu na vijiji vyao, maafisa wa Uganda karibu na mpaka katika mji wa Bungana wanasema.Mpigano yanakadiriwa kuwa kilometa 5 kutoka mpakani yalianza Alhamis usiku na inaripotiwa kuwa yanaendelea.
Idadi ya wakimbizi wa DRC nchini Rwanda imekuwa maradufu kwa wiki iliyopita kufikia 7,000 – na maelfu wengine wakimiminika katika kambi zilizo karibu na mji mkuu Goma.
Alhamis serikali katika ukanda huo zilisema baadhi ya watu walanza kurejea kwenye vijiji vyao wakati mapigano yalipositishwa, lakini mwandishi wa BBC Jonathan Kacelewa aliyeko eneohiloanasema watu bado wanayakimbia makaziyao.
Katika siku tano zilizopita kiasi cha askari 100 wa wapiganaji walirejea jeshini na rundo la silaha liligunduliwa, kwa muhibu wa msemaji wa Jeshi.
Inakadiriwa kuwa askari 900 walioasi bado hawajarejea, kwa mujibu wa vyanzo vya walioasi.
Kufuatia uasi uliotokea mwezi uliopita mapigano yalizidi katika eneo la Kivu ya Kaskazini
Kumekuwa na ukosoaji kutoka kwa makundi ya kiraia katika jimbo hilo kuwa makataa ya siku tano kumaliza mapigano yamewapa wapiganaji muda wa kujipanga upya.
No comments:
Post a Comment