Serikali ya Pakistan imesema
kuwa takriban wanamgambo wanane wameuawa kwenye shambulio la anga
lililofanywa na wanajeshi wa Marekani, karibu na mpaka wa Afghanistan.
Shambulio hilo, lilifanywa katika eneo la
Waziristan ya Kaskazini, eneo la kiuko ambalo ni ngome ya wapiganaji wa
Taleban na Al-Qaeda.Mwezi uliopita kamati ya bunge nchini Pakistan, alitoa wito wa kusitishwa kwa mashambulio hayo ya anga yanayotekelezwa na wanajeshi wa Marekani.
Wabunge hao walisema raia wengi wameuawa kwenye mashambulio hayo na kuwa yanakiuka uhuru wa taifa hilo.
No comments:
Post a Comment