Wednesday, May 23, 2012

Uchaguzi huru wa urais unafanyika Misri


Raia wa Misri wanajianda kushiriki katika uchaguzi wa kwanza huru tangu mapinduzi ya kiraia yaliomuondoa Rais Hosni Mubarak mamlakani miezi 15 iliopita.
Wapiga kura milioni 50 watashiriki katika uchaguzi huu ambao usalama unapewa kipa umbele.
Baraza kuu la jeshi nchini humo ambalo lilichukuwa utawala baada ya mapinduzi ya kiraia mwezi wa Februari mwaka jana, limeahidi kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki.
Nafasi ya urais imewavutia jumla ya wanasiasa 12, wenye itakadi kali za kidini, walio na msimamo wastani na mawaziri waliotumikia utawala wa aliyekuwa Rais Hosni Mubarak.
Mpiga kura nchini Misri
Wagombea wanaopewa nafasi nzuri kwenye uchaguzi huo ni Ahmed Shafiq, aliyekuwa kamanda wa jeshi la angani na Amr Moussa, aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje na kiongozi wa jumuiya ya nchi za kiarabu.
Wengine ni Mohammed Mursi, kiongozi wa vugu vugu la kiislamu, Muslim Brotherhood na Abdul Moneim Aboul Fotouh, mgombea binafsi lakini ambaye pia anegemea sera za kidini.
Uchaguzi huu utafanyika kwa siku mbili kutokana na idadi kubwa ya wapiga kura na ikiwa mshindi hatapatikana, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika j Juni tarehe 16 na 17.

Taarifa zinazohusiana

No comments:

Post a Comment