Thursday, May 17, 2012

KINACHOMTESA LULU NI HIKI



Na Richard Bukos
ITAKUMBUKWA kuwa Jumatatu iliyopita, mshitakiwa katika kesi ya kifo cha staa wa sinema za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘The Great’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ alitupiwa ombi lake la kutaka mahakama imtambue kuwa ana miaka 17 badala ya 18 ili kesi hiyo iendeshwe kwenye mahakama ya watoto.
Kesi hiyo ambayo iliunguruma Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mawakili wanaomtetea mshitakiwa huyo wakiongozwa na Kenedy Fungamtama waliwasilisha cheti cha kuzaliwa cha mlalamikiwa wao kinachoonesha ana miaka 17.
Hoja hiyo ilitupiliwa mbali na mawakili wa upande wa mashitaka waliokuwa wakiongozwa na mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo, Elizabeth Kaganda ambaye alisema cheti hicho kina dosari kadhaa.
Naye hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Augustine Mmbando alisema mahakama hiyo itaendelea kuutambua umri alioutaja mshitakiwa wakati akitoa maelezo yake polisi hadi pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
DOSARI YA KWANZA
Jina la mshitakiwa lilisomeka ni Diana Elizabeth Michael badala ya Elizabeth Michael. Mwendesha mashitaka huyo alisema jina hilo ni geni mahakamani hapo.
DOSARI YA PILI
Kaganda alisema mapungufu mengine ni cheti hicho kugandishwa kwenye nailoni (lamination) jambo ambalo halitakiwi kwenye uhifadhi wa vyeti.

KINACHOMTESA LULU
Kwa mujibu wa mazungumzo ya watu na wanasheria kadhaa, Lulu kwa sasa anateswa na mazingira aliyokuwa akiishi ambayo kwa sehemu kubwa yanapingana na umri unaotajwa.
Endapo msanii huyo angekuwa si maarufu, hakuna mtu ambaye angeibua utata wa umri wake kwa vigezo au ushahidi kama ilivyo sasa.
Kwa mujibu wa Kaganda, wakati akitoa maelezo kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar baada ya kukamatwa, Lulu alisema ana miaka 18 na aliambiwa ayapitie mara kadhaa maelezo yake kabla ya kuanguka sahihi.
Akizungumza baadaye, afisa mmoja mwandamizi wa mahakama hiyo alimwambia Kaganda:
“Wanasema Lulu ana umri wa miaka 17, mbona huwa anaonekana akiendesha magari, alipataje leseni akiwa na umri wa chini ya miaka 18?”
Kaganda: “Si ndiyo hapo sasa!”

SHEREHE YA BETHIDEI
Pamoja na malumbano hayo makali juu ya umri wa Lulu ndani ya mahakama hiyo, nje nako minong’ono ilishamiri. Sherehe yake ya kutimiza miaka 18 iliyoripotiwa kwenye vyombo vya habari, Aprili 2011 nayo ilitajwa.
“Halafu huyu Lulu si alishafanya bethidei ya kutimiza miaka 18 mwaka 2011, tena hata magazeti na kwenye mitandao waliandika,” alisema mtu mmoja nje ya mahakama hiyo.
“Nini kufanya bethidei, kwenye kipindi cha Mkasi alipohojiwa na Salma Jabir wiki moja tu kabla ya kifo cha Kanumba, Lulu alikiri ana miaka 18. Lakini pengine kweli, labda ni utoto ndiyo maana hana uhakika na umri wake,” alisema mwingine.

KUJIRUSHA KLABU
Aidha, minong’ono hiyo pia ilisikika ikijadili suala la msanii huyo kuwahi kuripotiwa (Machi 2011) kwamba alipigwa marufuku na mameneja wa klabu kubwa za usiku za jijini Dar kutokana na kuwa na umri mdogo, lakini baadaye mwenyewe akasema ‘amuone huyo wa kumkataza kuingia klabu.’
Wafuatiliaji hao walisema baada ya kutoa tamko hilo ndipo miezi michache mbele, Lulu akaangusha bethidei ya nguvu kwamba alitimiza miaka 18 hivyo alikuwa huru kuingia klabu kujirusha.
Walisema katika kujirusha kwake klabu, alisharipotiwa kuwa aliwahi kulewa chakari hadi nguo zikamvuka.

MADAI YA UHUSIANO NA ALI KIBA
Wapo pia waliokumbusha habari iliyowahi kuandikwa kwenye gazeti la Risasi la Septemba 4, 2010 ikiwa na kichwa cha kisemacho; ALI KIBA KUFIA JELA…endapo itathibitika Lulu ni mtoto mdogo (chini ya 18).
Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, msanii huyo wa Bongo Fleva alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lulu ambaye iliaminika ana miaka chini ya 18.
MAMA MZAZI ATETWA
Mama mzazi wa Lulu ameendelea kubebeshwa lawama kuhusu utata huo. Wengi walisema wakati mtoto wake anafanya bethidei kutimiza miaka 18 aliona au kusoma kwenye magazeti, kwa nini asipinge kama alijua amedanganya?
“Mama anasema mtoto wake ana miaka 17, siku zile anafanya bethidei mwanaye huyo alisema ametimiza miaka 18 kwa nini asipinge, ameona yaliyotokea sasa?” alihoji Mwantumu, mkazi wa Upanga, Dar.HABARI ZOTE NA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment