Historia
imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi msaada wa maboya (life
vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama
sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tangu Meli hiyo
ilipozama na kuua watu takriban 1,000 akiwemo pamoja na mama yake
Flaviana.
Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo.
---
Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kuokolea maisha ya watu katika vyombo vya usafiri wa majiambavyo
vimelengwa maalum kwa Ziwa Viktoria mjini Mwanza. Msaada wa vifaa hivyo
umeelekezwa katika shirika la kiserikali la usafiri wa majijijini
Mwanza lijulikanalo kama Marine Service Co. Ltd.
Flaviana
Matata ametoa jumla ya vifaa hivyo 500 (vyombo vya kuokoleamaisha ndani
ya maji) ikiwa ni kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MvBukoba mnamo Mei
21 mwaka 1996 ambapo pia alimpoteza mama yake mzazi katika ajali hiyo
iliyouwa watu takribani 1,000.
Sababu
mojawapo kubwa iliyofanya watu kupoteza maisha yao siku ya tukio hilo
ilikuwa upungufu na ukosefu wa vifaa vya majini kama maboya (Live Vest).
No comments:
Post a Comment