Kiongozi wa mashtaka katika
mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC Luis Moreno Ocampo ametoa ombi la
kukamatwa kwa kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kihutu la FDLR katika
eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sylvestre
Mudachumura.
Ocampo anasema kuwa Sylvestre Mudacumura, ni kiongozi wa waasi ambaye kwa sasa anahangaisha raia katika eneo la Mashariki mwa Congo.
Wote wawili sasa wanasakwa ili kujibu mashitaka uhalifu dhidi ya binadamu , uhalifu wa kivita, mauaji na ubakaji .
Bwana Moreno-Ocampo anasema kuwa Bosco Ntaganda na Sylvestre Mudachumura ni watu hatari zaidi na kuna ushahidi wa kutosha wa kuweza kuwapata wawili hao na hatia.
Hata hivyo mahakama ya ICC lazima impe Ocampo ruhusa ya kumuongezea mashitaka Ntaganda na pia kutaka Sylvestre Mudachumura akamatwe.
Mudacumura ndio mkuu wa FDLR, au wapiganaji wa ukombozi wa Rwanda. Viongozi wa kundi hilo inasadikiwa walishiriki katika mauji ya kimbari ya mwaka 1994.
No comments:
Post a Comment