Mwanamme anayeshutumiwa kupanga
mashambulio ya September 11 nchini Marekani, Khalid Sheikh Mohammed,
amefikishwa kwenye mahakama ya kijeshi katika kambi ya Guantanamo Bay.
Khalid Sheikh Mohammed na wenzake wane wanakabili mashtaka ya mauaji ya watu 2,976.
Sheria mpya zinakataza ushahidi uliopatikana kutokana na mateso, kama vile kumfanya mfungwa kama unamzamisha - mbinu iliyotumiwa sana na shirika la ujasusi la Marekani, CIA.
Mara ya kwanza kesi ya Khalid Sheikh Mohammed ilisimamishwa Rais Obama alipoingia madarakani.
Alitaka kesi hiyo ifanywe kwenye mahakama ya kiraia, lakini alizuwiliwa na upinzani bungeni.
No comments:
Post a Comment