Tuesday, May 8, 2012

KESI YA ELIZABETH MICHAEL (LULU) YAPIGWA KALENDA MPAKA MEI 21, 2012

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi  ametupilia mbali ombi la Mawakili watatu wanao mtetea a Muigizaji nyota wa Filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu (17) anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba, aliye fariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake maeneo ya Vatican Sinza Jijini Dar es Salaam.

Mawakili hao wanao mtete Lulu ni  Keneth Fungamtama, Fulgence Massawe, Peter Kibatala na Jackline De Meero.

Wakili  Fungamtama alidai Mahakamani hapo kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa wanaiomba Mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa Elizabeth kushitakiwa katika Mahakama ya watoto kwa kuwa ana umri chini ya miaka 18 pia kesi yake iwe INCAMERA.

Naye Wakili wa  Serikali Elizabeth Kaganda alidai  Mahakamani hapo kwamba  hawakubaliani na ombi hilo hivyo wanaomba wachunguze umri sahihi wa Elizabeth kwa upande wao ili ukweli uweze kubainika.

Kaganda alidai Mahakamani hapo kuwa umri wa Elizabeth unatatanisha kutokana na maelezo yanayotofautiana ya mtuhumiwa  huyo alyoyatoa awali  kwani alipohojiwa na Jeshi la Polisi alidai kuwa na umri wa miaka 17, pia majina yake katika cheti cha kuzaliwa ni Diana Elizabeth tofauti na linavyoandikwa katika kuwa Elizabeth Michael, upelelezi juu ya umri sahihi ni lazima.

 Lulu amepandishwa kizimbani  leo ikiwa  ni mara ya tatu sasa  ,mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya  Kisutu Jijini Dar es Salaam  Augustina Mmbando, Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo na amerudhishwa rumande.
Hakimu Mmbando alitupilia mbali ombi hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 196  kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai hivyo ameahirisha  kesi hiyo hadi Mei 21 mwaka huu  kesi hiyo itakapotajwa tena.

Tofauti na  hali ilivyokuwa  marambili ambapo  mtuhumiwa Lulu alipoletwa Mahakamani hapo ambapo watu walijazana na kuvuta hisia za wengi jana hakukuwa na mikiki ya aina yeyote ile hivyo lulu aliweza kuonekana bila taabu huku wanahabari wakiweza kufanya kazi kama kumpiga picha bila taabu yeyote bila kuzuiwa na Askari Magereza wala kukanyagana.

No comments:

Post a Comment