27 Mei, 2012 - Saa 10:50 GMT
Carl Froch amekua mtu wa tatu kushinda taji la dunia kwa kumzaba makonde ya kufululiza katika
raundi ya tano Lucian Bute kutoka Canada kwenye pambano lililofanyika
katika ukumbi wa Capital FM Arena mjini Nottingham,Uingereza.
Froch, mwenye umri wa miaka 34, hakutarajiwa kusimama kwa mda mbele ya bingwa huyu wa tawi la ndondi la IBF uzani wa Super Middle, Lucian mwenye sifa ya konde zito la kushoto.Hata hivyo ni Froch aliyeongoza kwa kushinda raundi mbili za kwanza kabla ya kumchapa vizuri katika raundi ya tatu ambapo bingwa alionekana akiyumbayumba sekunde chache kabla ya kengele kumuonkoa.
Raundi ya nne ilianza kwa Bute kujaribu kurejea katika pambano lakini dakika ya mwisho alimiminiwa makonde yaliyomlazimisha mwamuzi kusitisha pambano kwa mda na kuanza hesabu, lakini akavuka kigezo.
Lakini raundi ya tano, baada ya Froch kuona kua Bute ameiva vya kutosha akakiponda kichwa hadi mpinzani wake aliposalimu amri.
Baada ya pambano hili, Froch aliiambia BBC kua "baada ya kupoteza pambano langu dhidi ya Andre Ward kule Marekani nilijihisi nimedhalilika. Hivyo nilikuja hapa leo kubadili hali ya mambo.
Watu wengi walionelea kua nimekwisha.
Ushindi wa Froch unamuweka katika nafasi ya juu miongoni mwa mashujaa wa masumbwi wa Uingereza ikiwa ni mmoja wa wapiganaji bora wa uzani wa ratili 168 katika historia ya masumbwi Uingereza.
No comments:
Post a Comment