Maafisa wa serikali ya Pakistan wamesema kuwa aliyekuwa daktari wa Osama Bin Laden amehukumiwa miaka thelathini Gerezani.
Daktari huyo alituhumiwa kuwasaidia maafisa wa
ujasusi wa Marekani CIA kumsaka Osama Bin Laden na atahudumia kifungo
chake nchini Pakistan.Ripoti zinasema kuwa Shakil Afridi alipatikana na hatia ya uhaini.
Afridi anatuhumiwa kuendesha mradi bandia wa kutoa chanjo ambao unaaminika kusaidia maafisa wa CIA kumnasa Osama bin Laden katika maficho yake mjini Abottabad, ambako aliuawa na wanajeshi wa kitengo maalum cha marekani mwezi mei mwaka uliopita.
Waziri wa mambo ya nje wa marekani Bi Hillary Clinton, ametoa wito kwa serikali ya kuachiliwa kwa bwana Afridi, akisema kuwa kazi yake imekuwa na manufaa kwa serikali za Marekani na Pakistan.
No comments:
Post a Comment