Wednesday, May 9, 2012

BASI LA MURO LATEKETEA KWA MOTO MJINI MOROGORO


Basi la kampuni ya Kampuni ya Muro Investment, T820BEY lillilokuwa klikitokea Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam, limewaka moto na kuteketea  kabisa maeneo ya Maseyu Mkoani Morogoro. Ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 1:15 usiku Mei 8,2012, haikusababisha madhara kwa abiria isipokuwa mali zao zote ziliteketea kwa moto huo.

 Mmoja wa wahusika wa basi hilo alidai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika gari hilo. Inadaiwa kuwa gari hilo lilipata hitilafu katika taa na walipofika mjini Morogoro walifanyia marekebisho na kuendelea na safari na walipofika maeneo hayo ya Maseyu likashika moto.

 Magari yakipita pembeni ya basi hilo lililokuwa likiteketea kwa moto na hapakuwa na askari wala magari ya zima moto yaliyoweza kuwahi kufika na kuzima moto huo ulioliteketeza basi hilo kabisa.

No comments:

Post a Comment