Wachezaji wanaomzonga mwamuzi wakati wa mechi kupinga maamuzi kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Euro 2012 watarajie hatua kali, ameonya refa mkongwe Pierluigi Collina.
Collina amesema kua wachezaji pia wataonywa na kuadhibiwa endapo watazidi kushiriki malumbano na wachezaji wa upinzani.
Mizozano baina ya wachezaji ni suala ambalo tunataka lipigwe marufuku uwanjani. Hatutakia kuona wachezaji 20 wakianza malumbano. Wachezaji wenyewe wanafahamu, na hili si geni kwao, kwamba inapotokea malumbano uwanjani na kushiriki zaidi ya wachezaji kumi, kadi ya manjano sharti ionyeshwe.
Collina amesema kua wanafanya mazowezi ya mwili na visomo vikali vya uwanjani na kiakili kusaidia katika kufikia maamuzi mazuri na sawa wakati wa mashindano hususan juu ya kuchezeana vibaya.
Mojapo ya malengo ya yanayokusudiwa kufikiwa ndani ya viwanja ni kuwalinda wachezaji. Nidhamu pia ni sehemu ya ulinzi wa wachezaji.
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ya Euro 2012, yatakayoanza tarehe 8 Juni ndiyo mwanzo wa mpango wa UEFA kuendelea kujaribu matumizi ya maamuzi yasiyorisha kwa kutumia maofisa 8.
No comments:
Post a Comment