Tuesday, May 15, 2012

DIAMOND AANIKA YA WEMA NA JOKATE



Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Jokate.

Wema.
Na Mwandishi Wetu
STAA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, ameanika siri za warembo, Wema Sepetu na Jokate Mwegelo.
Diamond, amebainisha ubora wa warembo hao kimapenzi, huku akisisitiza kwamba mpenzi wake wa sasa, Jokate ni mzuri zaidi.
Kabla ya kudondokea kwa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili 2006-07, Diamond alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006-07.
Akizungumza mbele ya mama yake mzazi, Sanura Sami ‘Sandra’ huku paparazi wetu akishuhudia, Diamond alisema kuwa Jokate ni mwanamke bora tofauti na Wema.
Alisema: “Jokate ndiyo mke wangu. Ana akili sana huyu mwanamke.”
Aliendelea: “Jokate akisikia nina shoo, anahangaika kutafuta mavazi yatakayonifanya nipendeze. Tofauti na Jokate, Wema yeye muda umefika wa shoo, yeye anajipamba. Ukimwambia muda umekwenda anasema nimsibiri amalize kujipamba.
“Wema mbele ya Jokate ni mzigo. Jokate ana akili sana.”
Diamond, mbele ya mama yake, alikula kiapo kwa kutaja jina la Mungu kuwa kwa Jokate amefika na hatarajii kuachana naye.
Mwanamuziki huyo, aliwachambua warembo hao, wakati akieleza kufurahishwa na sare mfano wa zile za jeshi la polisi ambazo Jokate alimtengenezea maalum kwa ajili ya shoo ya Ukumbi wa Dar Live, iliyofanyika Aprili 29,2012...HABARI NA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment