Polisi wameimarisha doria hii
leo katika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini ambapo mahakama
inasubiriwa kutoa hukumu kwa vijana wawili wa Kiafrika wanaotuhumiwa
kumuua Eugene Terre' Blanche miaka miwili iliyopita.
Bwana Terre' blance alikuwa kiongozi wa mrengo
wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan
Resistance Movement.Wawili hao wamekanusha mashtaka ya kumuua muajiri wao na kutekeleza uwizi wa mabavu.
Mahlangu anadai kuwa alikuwa akijitetea ili hali mvulana anayeshtakiwa pamoja naye amekanusha kuhusika na uhalifu huo.
Kizingiti kikubwa katika kesi hii ni kuwa Mahlangu na mvulana huyo walikataa kutoa ushahidi wao, wakati wa kesi hiyo.
Hali ya wasi wasi inatarajiwa kutanda nje la makahakama hiyo kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo miaka miwili iliyopita.
Wakati huo, polisi walikabiliwa na wakati mgumu kuwatenganisha makundi ya wafuasi wa pande hizo mbili.
Lakini idara ya polisi na chama cha AWB zimesema kuwa ghasia zozote hazitarajiwi.
Polisi wamesema ikiwa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao, imeweka mikakati thabiti ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga shughuli za mahakama.
Mwezi uliopita, wakati mawakili walipokuwa wakitoa tetesi zao za mwisho mbele ya mahakama hiyo, jaji alionya kuwa hukumu huenda ikachukua muda mrefu lakini haijulikani, ikiwa uamuzi huo utachukua zaidi ya siku moja kutolewa.
Hata hivyo pande zote zinatarajiwa kukata rufaa baada ya hukumu kutolewa.
No comments:
Post a Comment